Tanzania, SA na Nigeria zawekewa marufuku ya usafiri Oman

Muhtasari

• Wasafiri wanaoingia Oman kutoka nchi 10 wamepigwa marufuku ya kuingia nchini humo.

Image: BBC

Wasafiri wanaoingia Oman kutoka nchi 10 wamepigwa marufuku ya kuingia nchini humo.

Nchi zilizopigwa marufuku ni Tanzania Afrika Kusini, Lebanon, Sudan, Brazil, Nigeria, Guinea, Ghana, Sierra Leone, na Ethiopia.

Marufuku hiyo itaanza kutekelezwa usiku wa Alhamisi wiki hii na itadumu kwa siku 15.

Hatua hiyo imetokana na maamuzi yaliyotolewa na kamati ya udhitibi wa Corona nchini humo.

Kamati hiyo imesema uamuzi huo ni wa kupambana na maambukizi ya Corona.

Marufuku hiyo pia inawahusisha watu watakaopita katika nchi hizo ndani ya siku 14 kabla ya kuingia Oman.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Oman, mkutano wa kamati hiyo uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Oman Hammoud bin Faisal Al Busaid.

Kamati hiyo imewataka wananchi wa Oman kutosafiri nje ya nchi ili kuzuia maambukizi na ikibidi kusafiri basi kuwe na sababu maalum.