Isaac Rutto; Singevumilia kuona Uhuru na Raila wakimpangia njama DP

Muhtasari

• Gavana huyo wa zamani wa Bomet alisema aliguswa na "mateso" yasiokuwa na sababu ambayo naibu rais Ruto alikuwa anapitia chini ya utawala.

 

Naibu rais William Ruto na mwenyekiti wa CCM Isaac Rutto
Naibu rais William Ruto na mwenyekiti wa CCM Isaac Rutto

Taarifa ya Gideon Keter 

Kinara wa chama cha CCM Isaac Rutto kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu uamuzi wake wa kumuunga mkono Naibu Rais William Ruto kuwa rais.

Gavana huyo wa zamani wa Bomet alisema aliguswa na "mateso" yasiokuwa na sababu ambayo naibu rais Ruto alikuwa anapitia chini ya utawala wa Jubilee na kiongozi wa ODM Raila Odinga.

Rutto ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Chama Cha Mashinani alifichua kwamba hatua yake ilifahamishwa na mateso ya Ruto.

 

Rutto alisema baada ya kumuunga mkono Raila katika uchaguzi wa 2017, alishangaa kwamba ushirikiano wake na Rais Uhuru umekuwa chanzo cha shida za naibu rais.

"Nilipoona kaka yangu (DP Ruto) ameachwa na kuteswa na utawala wa Jubilee akiwemo Odinga ambaye nilikuwa namuunga mkono, tulichagua kuungana ili kuwapinga," Rutto alisema.

Mbunge huyo wa zamani wa Chepalungu alisisitiza kwamba ushirikiano na Ruto-mpinzani wake mkuu katika kutafuta kudhibiti wa eneo la Bonde la Ufa - ulilenga kumkinga DP dhidi ya mateso ya kisiasa. 

Uhuru amekuwa akiongoza mashambulizi ya kisiasa dhidi ya Ruto baada kuibuka kwa mgawanyiko uongozi wa serikalini ya Jubilee.

Raila, kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi, kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka, mwenyekiti wa Kanu Gideon Moi na Moses Wetang'ula wa Ford Kenya wamempa rais Uhuru Kenyatta ujasiri wa kumkabili kisiasa Ruto.

Lakini Rutto, ambaye alifanya kazi na Raila, Kalonzo na Musalia chini ya muungano wa Nasa katika uchaguzi wa mwaka 2017, mwaka jana aliandika makubaliano ya ushirikiano na Jubilee, lakini ameamua kusimama na DP.

Mwishoni mwa wiki, Rutto alisimulia jinsi alivyogombana na vinara wenzake katika NASA licha ya kuwa katika mrengo mmoja 2017 na, kwa mshangao, alifichua kwamba hakutaka kumuacha DP.

 

Alisema kuwa alimwacha Raila kutokana na matokeo yake duni katika uchaguzi mkuu wa 2017.

Rutto alisema alikuwa na nia ya kumuunga mkono Odinga aingie madarakani dhidi ya Uhuru ambaye alikuwa akitafuta muhula wa pili.