3 wakamatwa na mbegu za wizi za shilingi milioni 7 zapatikana Narok

Mbegu ilionaswa katika bohari moja Narok
Mbegu ilionaswa katika bohari moja Narok

Washukiwa watatu wamekamatwa na zaidi ya marobota 1,700 ya mbegu zilizoidhinishwa za mahindi aina ya hybrid za Kampuni ya Kenya Seed, zenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni saba kupatikana kutoka ghala la kibinafsi katika kaunti ya Narok.

Brian Meja na wafanyabiashara wawili huko Narok wenye asili ya Asia wanaojulikana tu kama Yogesh na Gaurav walikamatwa Jumanne jioni.

Watatu hao walivamia kituo kilichokodishwa na Meja, umbali kidogo kutoka kbohari kuu la kampuni ya Kenya Seed, ambapo mbegu hizo za mahidi zilikuwa yamehifadhiwa.

Katika kile maafisa wa DCI walisema ni njama iliyopangwa sawa sawa, wapelelezi walibaini kuwa mbegu zilizoibiwa husafirishwa kwa magari mawili ya Probox kila siku na huhifadhiwa katika ghala la Meja kwa muda.

Hii ni kabla ya kuhamishiwa kwenye vituo vinavyomilikiwa na washukiwa wawili.

Takriban, marobota 40 kila moja yenye pakiti 12 za kilo 2 kwa kila pakiti, zimetolewa kila siku kwa wafanyabiashara hao wawili tangu mwezi Desemba mwaka jana.

Yogesh ambaye anamiliki bidhaa za Shakti Shamba na Ololulunga Shiv Agrovets katika mji wa Lulunga ana bohari nyingine moja ndani ya mji wa Narok ambayo kwa sasa imehifadhi zaidi ya tani 10 za begu zinazoshukiwa kuibwa.

Mtuhumiwa mwenzake Gurav anafanya kazi duka la Sai Agrovet huko Bomet.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa katika njama ya kuwalaghai wakulima walipakia mahidi ya kawaida waliopaka rangi na kuwauzia wakulima wasio fahamu kama mbegu halisi ya uzalishaji wa juu.

Mkurugenzi wa DCI George Kinoti alisema sampuli za mbegu zilizopatikana zitachunguzwa na wataalamu kutoka kwa Maabara ya Uchunguzi ya DCI, Mwanakemia wa Serikali na vyombo vingine vya serikali vinavyohusika kuimarisha kesi yetu dhidi ya wadanganyifu.