Covid-19:Wagonjwa 67 wapo katika kitengo cha ICU,400 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Wagonjwa 67  wapo katika kitengo cha ICU,400 wapatikana na corona
  • Huku hayi yakijiri watu 3 wameaga dunia kutokana na corona
Picha: REUTERS
Picha: REUTERS

Visa 400 vya corona vimeripotiwa nchini siku ya Jumatano baada ya sampuli 5,189 kupimwa katika saa 24 zilizopita .

Idadi hiyo inafikisha 107,729 jumla ya visa hivyo hadi sasa huku sampuli zilizopimwa zikifika 1,322,806.

Kutoka visa hivyo 367 ni wakenya ilhali raia wa kigeni ni 33 . mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 9 ilhali wa umri wa juu ana miaka 95.

 

Wagonjwa 248 ni wanaume huku 152wakiwa wanawake, kulingana na kaunti, kaunti ya Nairobi imeongoza kwa visa 279  vipya vya maabukizi ya corona ikifuatwa na kaunti ya Kiambu na visa 37.

Wagonjwa 77  wamepona ugonjwa huo huku idadi hiyo ikifika 87,176  Watu 27 wamepona wakipokea matibabu wakiwa nyumbani huku 50 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Watu 3  wamepoteza maisha yao kutokana na maradhi hayo na kufikisha idadi jumla 1,873 ya watu walioga dunia.

Kuna wagonjwa 494  ambao wamelazwa hospitalini ilhali 1,615  wapo chini ya mpango wa utunzi nyumbani .

Wagonjwa 67  wapo katika kitengo cha ICU.