Covid-19: Watu 465 wapatikana na corona,20 wapona,2 waaga dunia

Muhtasari
  • Wagonjwa 69 wapo katika kitengo cha ICU, huku wawili wakiaga dunia
  • Watu 465 wapatikana na corona huku 20 wakipona maradhi hayo
Picha: REUTERS
Picha: REUTERS

Visa 465  vya corona vimeripotiwa nchini siku ya Jumapili baada ya sampuli 5,691 kupimwa katika saa 24 zilizopita .

Idadi hiyo inafikisha 108,827 jumla ya visa hivyo hadi sasa huku sampuli zilizopimwa zikifika 1,333,690.

Kutoka visa hivyo 422 ni wakenya ilhali raia wa kigeni ni 43 . mgonjwa wa umri wa chini ana mwaka mmoja ilhali wa umri wa juu ana miaka 91.

 
 

Wagonjwa 279 ni wanaume huku 186 wakiwa wanawake, kulingana na kaunti, kaunti ya Nairobi imeongoza kwa visa 310 vipya vya maabukizi ya corona ikifuatwa na kaunti ya Kiambu na visa 58.

Wagonjwa 20 wamepona ugonjwa huo huku idadi hiyo ikifika 87,570 Watu 3 wamepona wakipokea matibabu wakiwa nyumbani huku 17 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Watu 2 wamepoteza maisha yao kutokana na corona na idadi hiyo kufika 18

Kuna wagonjwa 488 ambao wamelazwa hospitalini ilhali 1,394 wapo chini ya mpango wa utunzi nyumbani .

Wagonjwa 69 wapo katika kitengo cha ICU.