Covid-19: Watu 1,523 wapatikana na corona,18 waaga dunia

Muhtasari
  • Kenya imerekodi visa 1,523 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 7,423 katika muda wa saa 24 zilizopita
  • Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 3 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 105

Kenya imerekodi visa 1,523 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 7,423 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 141,365 kutoka kwa sampuli 1,530,736

Katika visa hivi vipya, 1,432 ni raia wa Kenya huku 91 wakiwa raia wa kigeni, 842 ni wa kiume na 681 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 3 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 105.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 616 wamepona virusi vya corona, 522 walipona wakiwa nyumbani huku 94 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 97,194 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 18 waliaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 2,276 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,591 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 6,112 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 236 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU)