Prince Philip:William na Harry kukutana katika mazishi ya babu yao

Muhtasari

• Watoto wake na wajukuu wanatarajiwa kuhudhuria, na Duke wa Sussex anaripotiwa kuwasili Uingereza kutoka Amerika kwa huduma hiyo.

• Prince Philip alifariki dunia katika kasri la Windsor siku uya ijumaa akiwa na umri wa miaka 99 .

 

Image: GETTY IMAGES

Watawala wa Cambridge na Sussex wametoa salamu za rambi rambi kwa babu yao, mtawala wa Edinburgh aliyefariki dunia siku ya ijumaa.

Katika taarifa tofauti, Prince William alimtaja kama "mtu wa kipekee", wakati Prince Harry alisema alikuwa "mtu wa huduma" .

"Nitamkosa Babu yangu, lakini najua angependa tuendelee na kazi hiyo," William aliongeza.

Prince Philip alifariki dunia katika kasri la Windsor siku uya ijumaa akiwa na umri wa miaka 99 .

Hilo linajiri wakati mabunge kote Uingereza yalirejelea vikao vyake ili kumkumbuka mtawala huyo.

"Karne ya maisha ya babu yangu imetambuliwa na huduma - kwa nchi yake na Jumuiya ya Madola, kwa mkewe na Malkia, na kwa familia yetu," Prince William alisema katika taarifa.

Mwanamfalme George na babu yake Mwanamfalme Philip
Mwanamfalme George na babu yake Mwanamfalme Philip
Image: THE DUCHESS OF CAMBRIDGE/PA MEDIA

"Ninajisikia mwenye bahati kuwa sio tu nilikuwa na mfano wake wa kuniongoza, lakini uwepo wake wa kudumu hata katika maisha yangu utu uzima - wakati wote mzuri na siku ngumu zaidi.

"Nitashukuru kila wakati kuwa mke wangu alikuwa na miaka mingi sana ya kumjua babu yangu na kwa wema aliomwonyesha.

"Sitawahi kuchukua kwa urahisi kumbukumbu maalum ambazo watoto wangu watakuwa nazo wakati wote wa babu yao kuja kuwachukua kwenye gari lake na kujionea hisia zake za urafiki na vile vile ucheshi wake!"

Aliongeza kuwa yeye na mkewe, Catherine, "wataendelea kufanya kile angekuwa anataka na watamuunga mkono Malkia katika miaka ijayo".

Mwanamfalme Harry na Mwanamfalme Philip walikua Makapteni wakuu wa jeshi la majini
Mwanamfalme Harry na Mwanamfalme Philip walikua Makapteni wakuu wa jeshi la majini
Image: GETTY IMAGES

Akitoa risala za rambi rambi kwa babu yake, Prince Harry alisema: "Alikuwa kwa kweli, mwenye busara kali, na angeweza kuwasisiumua watu sababu ya haiba yake - na pia kwa sababu hakujua nini atakachosema baadaye.

"Atakumbukwa kama mshirika wa kifalme aliyehudumu kwa muda mrefu mwanajeshi aliyepambwa na mataji ,mwanamfalme na mtawala mkuu'

Mazishi ya kifalme, ambayo yatapeperushwa kwa televisheni, yatafanyika kwa mtawala huyo huko St George's Chapel, katika uwanja wa Jumba la Windsor, saa 15:00 BST mnamo 17 Aprili.

Watoto wake na wajukuu wanatarajiwa kuhudhuria, na Duke wa Sussex anaripotiwa kuwasili Uingereza kutoka Amerika kwa huduma hiyo. Mkewe, Meghan, ambaye ni mjamzito, atabaki nyumbani California kwa ushauri wa madaktari.

Itakuwa mara ya kwanza Prince William na Prince Harry kukutana ana kwa ana tangu Harry alipoikosoa familia ya kifalme katika mahojiano na mtangazaji wa Marekani Oprah Winfrey mwezi uliopita.