Rais wa Somalia atia saini sheria kujiongezea hatamu

Muhtasari

 • Muhula wa miaka minne wa Rais Mohamed Abdullahi Mohamed ulimalizika mwezi Februari bila mrithi.

  • Wafadhili wakuu wa Somalia wanasema hawataunga mkono hatua ya kuongezwa kwa muda wowote.

Muhula wa Rais Mohamed Abdullahi Farmajo uliisha siku ya Jumatatu.
Muhula wa Rais Mohamed Abdullahi Farmajo uliisha siku ya Jumatatu.
Image: GETTY IMAGES

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi (Farmajo) ametia saini sheria yenye utata inayoongeza hatamu yake kwa miaka miwili zaidi, shirika la habari la serikali liliripoti.

Hatua hiyo imeliweka taifa hilo la upembe wa Afrika katika njia panda  na wafadhili ambao wanapinga vikali uamuzi huo.

"Rais Mohamed Abdullahi (Farmajo) leo usiku ametia saini mwelekeo wa mtu mmoja kura moja, sheria ambayo ilipitishwa kwa kauli moja na bunge mnamo Aprili 14," ilisema taarifa hiyo iliyotolewa na Waziri wa Habari Osman A Dubbe usiku wa Jumanne.

Muhula wa miaka minne wa Rais Mohamed Abdullahi Mohamed ulimalizika mwezi Februari bila mrithi.

Kiongozi mpya wa nchi hiyo alikusudiwa kuchaguliwa na wabunge wapya, lakini uteuzi wao ulicheleweshwa baada ya wapinzani kumshutumu rais kwa kujaza bodi za uchaguzi za mikoa na wafuasi wake.

Siku ya Jumatatu bunge la chini la Somalia lilipiga kura ya kuongeza muda wake lakini hatua hiyo ilikataliwa haraka na bunge la juu.

 Wafadhili wakuu wa Somalia wanasema hawataunga mkono hatua ya kuongezwa kwa muda wowote.

"Amerika imesikitishwa sana na uamuzi wa Serikali ya Somalia kuidhinisha muswada wa sheria ambao unamuongezea hatamu rais na bunge kwa miaka miwili," ilisema taarifa ya Jumanne ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony J. Blinken.

"Italazimisha Amerika kutathmini upya uhusiano wetu wa pande mbili na Serikali ya Somalia, kujumuisha ushirikiano wa kidiplomasia na ufadhili, na kuzingatia zana zote zilizopo, pamoja na vikwazo na marufuku ya viza."