• Urusi imesema itazuia safari za ndege kwenda Uturuki na Tanzania kuanzia Aprili tarehe 15 hadi Juni tarehe 1 kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona
Urusi imesema itazuia safari za ndege kwenda Uturuki na Tanzania kuanzia Aprili tarehe 15 hadi Juni tarehe 1 kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona nchini humo , Naibu Waziri Mkuu Tatiana Golikova amesema .
Kumekuwa taharuki ya kisiasa kati ya Urusi na Uturuki ambayo inategema pakubwa mapato ya utalii kutpoaka wageni wa Urusi.
Uamuzi huo unajiri siku mbili tu baada ya rais Tayyip Erdogan kukutana na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy huko Istanbul.
Kulingana na shirika la habari la Reuters Urusi pia imesitisha safari za kwenda nchini Tanzania kuanzia Aprili tarehe 15 hadi Juni tarehe 1.
Hata hivyo waziri wa Utalii wa Zanzibar Leila Mohamed Musa ameiambia BBC kwamba hawajapokea taaroifa rasmi kuhusu uamuzi huo wa Urusi na wameahidiwa kupewa jibu na Ubalozi wa Urusi nchini humo .