KCPE! matokeo ya mtihani wa kitaifa kutolewa leo

Muhtasari

• Waziri wa Elimu George Magoha yuko tayari kutangaza matokeo ya mtihani huo.

• Mtihani wa KCPE ulicheleweshwa kutokana na janga la Covid-19.

Waziri wa Elimu George Magoha

Watahiniwa wa mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE wanatarajiwa kujua matokeo yao hivi leo.

Waziri wa Elimu George Magoha yuko tayari kutangaza matokeo ya mtihani huo.

Mtihani wa KCPE ulicheleweshwa kutokana na janga la Covid-19.

Magoha atakutana na Rais Uhuru Kenyatta kwanza katika Ikulu kwa ajili ya kumkabidhi rais ripoti ya matokeo mtihani wa KCPE mwaka wa 2020 kabla ya matokeo hayo kutangazwa rasmi.

kcpe
kcpe

Mtihani wa KCPE wa 2020 ulianza Machi 22 na kumalizika Machi 24, na maandalizi yalifanywa Machi 19.

Watahiniwa 1,181,725 ​​walifanya mtihani huo, na kuashiria ongezeko kutoka 1,083,456 waliofanya mtihani huo mwaka 2019.

Kati ya wasichana 3,500 katika shule za msingi waliopatikana na ujauzito, zaidi ya watahiniwa 200 kati yao walifanya mtihani huo.

Mwezi uliopita, katibu wa kudumu wa Elimu ya Msingi Julius Jwan alisema kwamba kusahihishwa kwa mtihani huo kulikuwa kunafanywa na walimu waliopewa kandarasi na Baraza la Mitihani nchini (KNEC).