Orodha ya wanafunzi ambao wameongoza katika mtihani wa KCPE

Muhtasari

Waziri wa Elimu George Magoha Alhamisi, Aprili 15, ametangaza matokeo ya mtihani wa shule za msingi (KCPE) huko Mtihani House jijini Nairobi

CS magoha
CS magoha

Waziri wa Elimu George Magoha Alhamisi, Aprili 15, ametangaza matokeo ya mtihani wa shule za msingi (KCPE) huko Mtihani House jijini Nairobi.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Magoha alibaini kuwa utendaji wa jumla katika 2020 uliboreshwa ikilinganishwa na ile ya 2019.

Mwanafunzi Mumo Faith Kawi alipata alama 433 ikilinganishwa na alama 440 zilizopatikana na mnafunzi wa 2019.

 

Wesonga Yuvet Nanzala na Murithii Angel Gakenia walipata alama 432, wakifuatiwa na Samuel Wanyonyi 431, Castro William 431, Maureen Tarus 431, Abiud Kipkurui 430, Margaret Mwangi 430, Dennis Omondi 429, Joyce Nkatha 429.

Watahiniwa milioni 1,179,182 walifanya mtihani wa KCPE kati ya Machi 22 na Machi 24, 2021. Watahiniwa 590,450 wa KCPE 2020 walikuwa wavulana wanaowakilisha 50.07% na 588,742 walikuwa wasichana wanaowakilisha 49.93%.