Mama na mwanawe wakamatwa na silaha kali Dagoreti

Muhtasari

• Silaha zilizonaswa ni bunduki aina ya M4 yenye uwezo wa kurusha risasi kwa umbali wa mita 500, bastola nne, bunduki aina ya submachine gun yenye uwezo wa kurusha risasi 600 kwa dakika na risasi 3,700 .

Bunduki zilizonaswa
Bunduki zilizonaswa
Image: DCI

Polisi wameshangazwa na kunaswa kwa bunduki kadhaa na risasi kutoka kwa wanawake wawili mtaani Dagoretti, Nairobi.

Silaha hizo, ambazo zilijumuisha bunduki aina ya M4 yenye uwezo wa kurusha risasi kwa umbali wa mita 500, bastola nne, bunduki aina ya submachine gun yenye uwezo wa kurusha risasi 600 kwa dakika na risasi 3,700 za aina tofauti zilipatikana siku ya Jumatano alasiri katika operesheni ya polisi.

Image: DCI

Polisi walisema waliwakamata wanawake wawili- Joyce Muthoni Mwihia na mamake Goretti Mwihia - ambao wanashikilia uraia wa nchi mbili Kenya na Amerika na ambao wanaishi Racecourse, Dagoretti Corner, Nairobi.

"Bado hatujajua nia ya wawili hao na bado tunachunguza suala hilo," polisi walisema.

Wanawake hao walichukuliwa kuhojiwa na maafisa kutoka Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Ugaidi.

Mkuu wa ATPU John Gachomo alisema walikuwa wamepeleka silaha hizo kwa wataalam kwa uchunguzi.

Aliongeza kuwa silaha hizo zinaonekana kuingizwa nchini kinyume cha sheria.

Image: DCI

Wawili hao wanatarajiwa kortini Alhamisi wakati polisi wakichunguza uwezekano wao kuwa na uhusiano na shughuli za kigaidi.