Baa kufungwa saa moja usiku,kafyu kuanzia saa nne usiku kote nchini

Muhtasari
  • Baa kufunguliwa hadi saa moja usiku,kafyu kuanzia saa nne usiku kote nchini

Rais Uhuru Kenyatta akihutubia taifa siku ya sikukuu ya labour day, amesema kwamba baa zote kufunguliwa hadi saa moja usiku.

Pia rais amesema kwamba kafyu itaanza kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri nchini kote.

Uhuru ameongeza muda wa  amri ya kuingia na kutoka katika kaunti tano alizoweka vikwazo vipya.

Kaunti hizo tani ni pamoja na Nairobi, Kajiado,Nakuru,Kiambu na Machakos.

Muda wa kafyu katika kauntti hizo tano utaanza kuanzia saa nne, na kutoa alivyoweka kuanzia saa mbili usiku.

Rais amesema kwamba ameamua hayo baada ya maambukizi ya corona kuteremka.

Mengi yafuata;