Rais wa LSK Nelson Havi asema hatamuomba Martha Koome msamaha

Muhtasari

Katika barua kujibu madai ya mawakili wa Koome kwamba aombe msamaha au kushtakiwa kwa madai ya kuharibia jina Koome, Havi alisema maoni yake kuhusu jaji huyo yalikuwa kwa masilahi ya umma.

Rais wa LSK Nelson Havi
Rais wa LSK Nelson Havi Rais wa LSK Nelson Havi

Rais wa Chama cha Wanasheria wa Kenya Nelson Havi hataondoa madai yake kwa JSC dhidi ya Jaji mkuu mteule Martha Koome wala kumuomba msamaha.

Katika barua kujibu madai ya mawakili wa Koome kwamba aombe msamaha au kushtakiwa kwa madai ya kuharibia jina Koome, Havi alisema maoni yake kuhusu jaji huyo yalikuwa kwa masilahi ya umma.

Wiki iliyopita, Koome alikuwa amemwambia Havi kwamba atamshtaki kwa "aibu, kejeli, na kumdhalilisha" kutokana na waraka ambao ulikuwa umewasilishwa na Havi kwa Tume ya Huduma ya Mahakama ikimtuhumu kwa kukosa uwezo wa kuwa jaji huru bila muingilio wa serikali.

 

Havi alikuwa amehoji uwezo wa Jaji koome kutokuwa na upendeleo,  maamuzi huru na uadilifu wake. Alisema hulka yake inamfanya ashindwe kuzuia ushawishi, haswa kutoka kwa serikali, na kufanya maamuzi huru.

Jaji wa mahakama ya rufaa Martha Koome alipofika mbele ya JSC kuhojiwa kuhusu wadhifa wa jaji mkuu, 14/04/2021.
Jaji wa mahakama ya rufaa Martha Koome alipofika mbele ya JSC kuhojiwa kuhusu wadhifa wa jaji mkuu, 14/04/2021.
Image: CHARLENE MALWA

Koome alilalamika kuwa madai ya Havi yalikuwa ya kumharibia jina na kwamba atamshtaki.

Lakini rais wa LSK siku ya Jumatatu alisema vitisho vya Koome kumshtaki wakati anafanya kazi yake rasmi ni ushauri mbaya na alionyesha kuwa "hata uthabiti wa kushikilia uzito wa ofisi" anayotarajiwa kuchukua.

Havi anadai kwamba vitisho vya jaji vinalenga kubana sauti yake kutowasilisha hati hiyo hiyo au nyingine yoyote kumhusu kwa Bunge, ambalo tayari limetaka umma kuwasilisha nyaraka zao dhidi ya Koome wakati wa kupigwa msasa.

Aliendelea kuhoji uaminifu wa Koome, akisema kwamba hata bodi ya kuwapiga msasa majaji ilimruhusu aendelee kuhudumu kama jaji kwa tundu la sindani.

"Hakuna kinachoonyesha kuwa ameboresha uadilifu wake kuendelea kuhudumu, alisema. Ikiwezekana kwamba Koome anachagua kumshtaki, anapaswa kumkabidhi malalamishi yake  mwenyewe," alisema.