Gavana wa Wajir Mohamed Abdi apigania kiti chake mbele ya seneti

Muhtasari

• Mawakili wa pande zote mbili, (upande wa Gavana na upande wa bunge la kaunti) walifika mbele ya kamati ya seneti ya wanachama 11 inayosikiliza madi dhidi yake.

• Gavana huyo atawakilishwa na timu ya mawakili wakiongozwa na Paul Nyomodi na Ndegwa Njeru.

Gavana wa Wajir Mohamed Abdi
Gavana wa Wajir Mohamed Abdi
Image: MAKTABA

Gavana wa Wajir Mohamed Abdi amejiwasisha mbele ya seneti kujitetea kwa lengo la kuokoa wadhifa wake baada ya bunge la kaunti kupitisha kura ya kumuondoa afisini.

Kikao cha kusikiza madai dhidi ya Gavana Abdi kilianza asubuhi siku ya Jumatano katika Seneti.

Mawakili wa pande zote mbili, (upande wa Gavana na upande wa bunge la kaunti) walifika mbele ya kamati ya seneti ya wanachama 11 inayosikiliza madi dhidi yake.

Gavana huyo atawakilishwa na timu ya mawakili wakiongozwa na Paul Nyomodi na Ndegwa Njeru.

Upande wa bunge la kaunti unawakilishwa na Wakili Mwandamizi Ahmednasir Abdullahi.

Pande zote zimepanga mashahidi watatu kila mmoja kama ilivyoelekezwa na kamati.

Mwenyekiti Okong'o Omogeni (seneta wa Nyamira) alisoma kanuni za msingi na kuamuru karani aanze kusoma mashtaka dhidi ya gavana Mohamed Abdi.