Sammy Leshore kuchukua nafasi ya Isaac Mwaura katika seneti

Muhtasari

• Mbunge wa zamani Sammy Leshore ametangazwa katika gazeti rasmi la  serikali kama atakayechukuwqa wadhifa wa Isaac Mwaura kama seneta maalum.

• Mwaura hata hivyo tayari amepata agizo la mahakama linalomzuia Spika wa Seneti Kenneth Lusaka kutangaza kiti chake wazi.

Sammy Prisa Leshore achapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali kuchukuwa nafasi ya Isaac Mwaura katika seneti.
Sammy Prisa Leshore achapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali kuchukuwa nafasi ya Isaac Mwaura katika seneti.

Mbunge wa zamani Sammy Leshore ametangazwa katika gazeti rasmi la  serikali kama atakayechukuwqa wadhifa wa Isaac Mwaura kama seneta maalum.

Leshore ni seneta wa zamani wa Samburu.

Mwaura hata hivyo tayari amepata agizo la mahakama linalomzuia Spika wa Seneti Kenneth Lusaka kutangaza kiti chake wazi.

Jumanne jioni, mahakama ilisimamisha kuondolewa kwake ikisubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa rufaa aliowasilisha.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Mei 24.

Jaji wa Mahakama ya Milimani J.K Sergon alitoa agizo la kuzuia utekelezaji wa uamuzi wa Mahakama ya Vyama vya Kisiasa uliyotolewa Mei 7, 2021, hadi kesi hiyo itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Mwaura aliwahi kuhudumu kama mbunge maalum baada ya kuteuliwa na chama cha ODM mwaka 2012, kabla ya kuhamia Jubilee na kuteuliwa tena kama seneta maalum.

Alifurushwa na chama tawala cha Jubilee kwa madi ya utovu wa nidhamu.