Watu Zaidi wauawa huku Israel na Hamas zikizidisha mashambulizi

Muhtasari

• Israeli inasema imefikia malengo 150 huko Gaza kujibu mashambulizi hayo. 

• Maafisa wa afya wanasema Wapalestina 28 wameuawa.

Image: REUTERS

Kumekuwa na majeruhi zaidi huko Gaza na Israeli, wakati mashambulizi mazito kati ya wanamgambo wa Palestina na jeshi la Israeli yakiendelea.

Wapiganaji wamefyatua makombora zaidi ya 300 kuelekea Israeli tangu Jumatatu usiku, na kuwaua Waisraeli wawili.

Israeli inasema imefikia malengo 150 huko Gaza kujibu mashambulizi hayo. Maafisa wa afya wanasema Wapalestina 28 wameuawa.

Jumuiya ya kimataifa imezitaka pande zote mbili kukomesha kuongezeka kwa machafuko ambayo yanafuata siku kadhaa za vurugu huko Jerusalem.

Kikundi cha wanamgambo cha Hamas, kinachodhibiti Gaza, kilisema kilikuwa kikijitetea kulinda msikiti wa al-Aqsa wa Jerusalem kutoka kwa "uchokozi na ugaidi" wa Israeli baada ya eneo hilo, ambalo ni takatifu kwa Waislamu na Wayahudi, kushuhudia mapigano kati ya polisi wa Israeli na Wapalestina Jumatatu ambayo yalisababisha mamia kujeruhiwa.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alisema Hamas "imevuka mstari mwekundu" kwa kurusha roketi kuelekea Jerusalem kwa mara ya kwanza kwa miaka.

Baada ya kukutana na wakuu wa kijeshi Jumanne alasiri, Bw Netanyahu alionya kwamba wamekubali kuongeza nguvu ya mashambulizi Gaza, na kuongeza kuwa Hamas "itapigwa kwa njia ambayo haitarajii".

Siku chache zilizopita zimeshuhudia ghasia mbaya kabisa huko Yerusalemu tangu 2017.

Ilifuata kuongezeka kwa hasira ya Wapalestina juu ya hofu ya kufurushwa kwa familia kutoka kwa nyumba zao huko Jerusalem Mashariki iliyokaliwa na walowezi wa Kiyahudi, iliyosababishwa na mzozo wa mwezi mmoja kati ya waandamanaji na polisi katika sehemu kubwa ya Waarabu.

Image: GETTY IMAGES

Kumekuwa na wito wa kudumisha utulivu siku kadhaa baada ya kutokea kwa machafuko huko Jerusalem katika mashambulizi ya kulipiza kisasi kati ya Israel na wanamgambo wa Palestina huko Gaza.

Marekani, Umoja wa Ulaya na Uingereza zimetoa wito kwa pande zote mbili kujizuia kuzua wasiwasi kadiri ya uwezo wao.

Wanamgambo wamefyatua zaidi ya roketi 300 kuelekea Israel tangu Jumatatu usiku na kujeruhi raia 31 wa Israel.

Israel nayo imesema mashambulizi yake ya anga huko Gaza yamelenga maeneo 130 huku maafisa wa afya wakithibitisha kuwa raia 24 wa Palestina wameuawa.

Kundi la wanamgabo la Hamas, ambalo linadhibiti eneo la Palestina lilisema limechukua hatua kulinda msikiti wa al-Aqsa ulipo Jerusalem dhidi ya "uchokozi na ugaidi" baada ya kutokea kwa mapigano kati ya polisi wa Israeli na Wapalestina kwenye eneo hilo ambalo ni takatifu kwa Waislamu na Wayahudi na kusababisha mamia ya watu kujeruhiwa.

Waziri Mkuu wa Israelir Benjamin Netanyahu kusema kuwa kundi la Hamas "limevuka mpaka" kwa kitendo chao cha kufyatua roketi kuelekea upande wa Jerusalem kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mingi na kuwa Israel itajibu "vikali" shambulizi hilo kwa nguvu kubwa".

Siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa ghasia baya zaidi huko Jerusalem tangu mwaka 2017.

Hali ikoje sasa hivi?

Vurugu hizo zimeendelea usiku mzima huku sauti za roketi za Palestina na mashambulizi ya anga yanayotekelezwa na Israeli yakitanda kote Jumanne asubuhi.

Kufikia alfajiri, roketi zilikuwa zimepiga nyumba mbili kusini mwa mji wa Israel wa Ashkelon.

Madaktari wa Israel walisema kuwa watu 31 wamejeruhiwa wakiwa ni pamoja na mwanamume wa miaka 40, ambaye alipata majeraha ya kichwa na yuko hali mahututi hospitali. Mke wake na watoto wake pia walijeruhiwa.

Upande wa Hamas umesema umepiga roketi eneo la Ashkelon kujibu shambulizi la anga lililotekelezwa na Israel ambalo lililenga nyumba ya komanda wao mkuu.

Image: REUTERS

Pia kundi hilo limetishia kubadilisha mji huo kuwa "jehanami" ikiwa raia wa Palestina wataendelea kulengwa.

Jeshi la Israel limesema limeshambulia maeneo 130 waliolenga huko Gaza usiku, ikijibu mashambulizi mawili kwenye handaki linalochimbwa chini ya mpaka na Israel, kituo cha kijasusi cha Hamas na ameneo ya kutengeneza na uhifadhi wa silaha.

"Tumedhamiria kuendelea kushambulia Hamas na vituo vyao vyote vya kijeshi kwasababu ya uchokozi wao dhidi ya Israel," msemaji luteni kanali Jonathan Conricus ameeleza BBC.

Imesema kuwa mwanamke mmoja, 59, na kijana wake mlemavu wamefariki dunia kaatika shambulo Jumanne asubuhi.

Jumatatu usiku, watu saba wa familia moja wakiwemo watoto watatu walifariki dunia katika mlipuko uliotokea mji wa Beit Hanoun.

Ulimwelingu umejibu vipi ?

Kupitia ujumbe wa Twitter, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Dominic Raab alisema kuwa mashambulizi ya roketi "lazima yasitishwe", na kutoa wito wa "kusitisha ulengaji wa raia".

Msemaji wa EU wa masuala ya mambo ya nje, Josep Borrell, alisea "kuongezeka kwa kiwasi kikubwa kwa ghasia" katika ukingo wa Magharibi, Gaza na Jerusalem Mashariki "kusitishwe mara moja".

"Kurushwa kwa roketi kutoka upande wa Gaza dhidi ya raia wa Israel ni kitendo kisichokubalika kabisa," msemaji amesema.

Image: EPA

Aidha, msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kutetea haki za binadamu, Rupert Colville, alisema "ina wasiwasi mkubwa" kutokana na ghasia hizo zinazozidi kuongezeka na kushutumu"vichocheo vyote vya ghasia na mgawanyiko wa kikabila na vitendo vya kichokozi".

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya mkutano wa dharura Jumatatu kujadiliana hali hiyo lakini halikutoa tamko lolote.

Afisa wa Palestina ameliambia shirika la Reuters kuwa UN, Misri na Qatar ambazo mara nyingi huwa zinakuwa mpatanishi kati ya Israel na kundi la Hamas, zote zinajitahidi kwa kila namna kusitisha mapigano hayo.

Ghasia hizo zimesababishwa na nini?

Mapigano kati ya Israel na kundi la Hamas yalisababishwa na siku kadhaa za mapigano kati ya Wapalestina na polisi wa Israel kwenye eneo takatifu la Mashariki mwa Jerusalem.

Al-Aqsa ni jina la msikiti uliopo katika ardhi yenye ekari 35 na hufahamika na Waislamu kama al-Haram al-Sharif, huku Wayahusi wakiuita Hekalu.

Msikiti huo usio wa kawaida upo mjini Jerusalem na ni eneo ambalo limeorodheshwa miongoni mwa turathi za kitaifa na shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu utamaduni UNESCO.

Eneo la msikiti huo ndilo lenye utata zaidi duniani tangu 1967 wakati Israel ilipokalia eneo la mashariki mwa Jerusalem ikiwemo eneo la zamani la mji huo.

Msikiti wa Al-Aqsa Jerusalem
Msikiti wa Al-Aqsa Jerusalem
Image: AFP

Mgogoro huo ulianza zama za kale kabla ya kuzaliwa kwa taifa la Israel.

Kwa Waislamu , msikiti wa al-Aqsa uliopo mjini Jerusalem ndio eneo la tatu kwa utakatifu.

Msikiti wa Al Aqsa ndio uliokuwa ukitumiwa kama qibla{Eneo ambalo Waislamu hutazama wanaposali} kwanza kabla ya kibla kwenda Mecca.

Ukarabati wa jengo hilo uliofanyika katika karne ya 7 , unaaminika na Waislamu kuwa eneo ambalo Mtume Muhammad alipaa mbinguni.

Wayahudi wanaamini kwamba jengo hilo takatifu , mara ya kwanza lilikuwa hekalu lao, lakini sheria ya Kiyahudi inapinga kuingia na kuomba kwa kuwa ni eneo takatifu sana.

Ukuta ulioko magharibi mwa msikiti huo unajulikana na Wayahudi kama ukuta wa maombolezo, unaodaiwa kuwa ukuta uliosalia wa hekalu hilo la Wayahudi.