Jaji Mkuu mteule Martha Koome afika bungeni kupigwa msasa

Muhtasari

• Kamati ya bunge ya sheria inatarajiwa baada ya kumhoji Koome kuwasilisha ripoti yake kwa bunge kuidhinisha au kukataa pendekezo la JSC.

• Kwa sasa naibu jaji mkuu Philomena Mwilu ndiye kaimu Jaji Mkuu wadhifa ambao anatarajiwa kundelea kushikilia hadi pale jaji  mkuu takapo teuliwa.

Jaji wa mahakama ya rufaa Martha Koome alipofika mbele ya JSC kuhojiwa kuhusu wadhifa wa jaji mkuu, 14/04/2021.
Jaji wa mahakama ya rufaa Martha Koome alipofika mbele ya JSC kuhojiwa kuhusu wadhifa wa jaji mkuu, 14/04/2021.
Image: CHARLENE MALWA

Jaji Martha Koome aliyependekezwa na tume ya Huduma kwa mahakama JSC kwa wadhifa wa Jaji Mkuu leo Alhamisi amefika mbele ya kamati ya bunge ya maswala ya kisheria kuhojiwa kuhusu uteuzi wake.

Kamati hiyo inatarajiwa baada ya kumhoji Koome kuwasilisha ripoti yake kwa bunge kuidhinisha au kukataa pendekezo la JSC.

Ikiwa bunge litaidhinisha pendekezo hilo basi jina la Martha Koome litawasilishwa kwa rais Uhuru Kenyatta kumteua rasmi kama Jaji mkuu baada ya kuapishwa.

JSC mnamo Aprili 27 ilipendekeza Martha Koome kuwa jaji mkuu wa Kenya kuchukuwa nafasi iliyowachwa wazi na David Maraga aliyestaafu mapema mwaka huu. Mwenyekiti wa JSC Prof Olive Mugenda alitangaza kuwa tume hiyo ilikuwa imekubali kwa kauli moja kumpendekeza Koome kuwa Jaji Mkuu.

Rais wa mahakama ya rufaa Jaji William Ouko pia alipendekezwa na JSC kwa wadhifa wa jaji wa mahakama ya upeo kuchukuwa nafasi ya JB Ojwang aliyestaafu.

Kwa sasa naibu jaji mkuu Philomena Mwilu ndiye kaimu Jaji Mkuu wadhifa ambao anatarajiwa kundelea kushikilia hadi pale jaji  mkuu takapo teuliwa.