Kwa nini wimbi jipya la mzozo Jerusalem na Gaza halikuweza 'kuepukika'?

Muhtasari

• Kuzuka kwa ghasia kati ya Waisraeli na Wapalestina kumesababisha takriban watu 230 kufariki katika eneo la Gaza na watatu nchini Israel.

• Kuzuka kwa ghasia wakati huu kumekuwa ukumbusho kwamba matukio mjini Jerusalem na maeneo matakatifu yamekuwa na uwezo wa kuchochea wengi.

Hamas ilirusha mabomu mengi ya roketi katika miji tofauti ya Israel
Hamas ilirusha mabomu mengi ya roketi katika miji tofauti ya Israel
Image: AFP

Wimbi jipya la ghasia limekumba Israel na ukanda wa Gaza, huku matatizo ya jadi kati ya Wayahudi na Waarabu ambayo yameendelea kuathiri eneo hilo yakikosa utatuzi.

Ni kidonda kilicho wazi katikati mwa eneo la mashariki ya kati na kwamba licha ya kwamba mzozo huo haujakuwa katika vichwa vya habari vya kimataifa katika miaka ya hivi karibuni haimanishi kwamba ulikuwa umekwisha.

Matatizo hayabadiliki, huku chuki na uchungu ukiendelea kukumba hata kizazi kijacho.

Kuzuka kwa ghasia kati ya Waisraeli na Wapalestina kumesababisha takriban watu 230 kufariki katika eneo la Gaza na watatu nchini Israel.

Chanzo cha mzozo

Kwa zaidi ya karne moja sasa , Wayahudi na Waarabu wamekuwa wakipigania kumiliki ardhi kati ya mto Jordan na bahari ya shamu.

Israel imewaadhibu Wapalestina tangu taifa hilo lilipobuniwa 1948, lakini haiwezi kujitangaza kuwa mshindi.

Na iwapo mgogoro huo utaendelea hakuna aliye na hakika ni nani atakayekuwa mshindi..

Hali ya wasiwasi ilikuwa imetanda kwa wiki kadhaa
Hali ya wasiwasi ilikuwa imetanda kwa wiki kadhaa
Image: REUTERS

Hakikisho lilipo ni kwamba kila miaka michache ijayo kutakuwa na mgogoro mbaya zaidi.

Mfumo uliopo katika kipindi cha miaka 25 iliopita umehusisha vita katika uwa wa waya unaotenganisha Gaza kutoka kwa Israel.

Tatizo la Jerusalem

Kuzuka kwa ghasia wakati huu kumekuwa ukumbusho kwamba matukio mjini Jerusalem na maeneo matakatifu yamekuwa na uwezo wa kuchochea wengi.

Utakatifu wa mji huo kwa upande wa Wakristo , Wayahudi na Waislamu sio tu swali la kidini.

Maeneo matakatifu ya Waislamu na Wayahudi pia ni maeneo ya kitaifa.

Hekalu la mlimani

Kijiografia ni halisi kwamba maeneo hayo yako kandokando.

Kanisa la mtakatifu Sepulcher pia liko karibu, karibu na kizuizi cha Israel, kinachoheshimiwa na Wakristo wa Palestina.

Kipi kipya hivi sasa?

Kumekuwa na tishio la kuwafurusha Wapalestina kutoka katika makaazi yao katika wilaya ya Sheikh Jarrah.

Ni eneo la Palestina nje ya ukuta wa mji wa zamani, huku ardhi `na mali zikimilikiwa na Walowezi katika mahakama za Israel.

Ni eneo lenye mzozo wa umiliki wa makazi machache.

Hatua hiyo inajiri baada ya miaka kadhaa ya serikali zilizopita zenye lengo la kuhakikisha kuwa Jerusalem ni ya Wayahudi.

Makazi ya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi inayomilikiwa na Wapalestina yamekuwa yakiongezeka
Makazi ya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi inayomilikiwa na Wapalestina yamekuwa yakiongezeka
Image: REUTERS

Makazi makubwa ya Wayahudi yalijengwa kwenye ardhi iliyokaliwa ili kuuzunguka mji, kwa lengo la kukiuka sheria za kimataifa.

Katika miaka ya hivi karibuni, serikali na vikundi vya walowezi vimefanya kazi kuwapatia makaazi Wayahudi wa Israeli katika maeneo ya Wapalestina karibu na Jiji la Kale kutoka nyumba moja hadi nyingine.

Cheche mpya

Hizi zilitiliwa mafuta katika wiki za hivi karibuni kufuatia hatua ya Israel kuwasimamia na ukali Wapalestina wakati wa mwezi wa Ramadhan , hatua iliosababisha maji ya pilipili na vitoa machozi kurushwa ndani ya msikiti wa al-Aqsa, eneo ambalo ni takatifu zaidi miongoni mwa waumini wa dini ya Kiislamu baada ya Mecca na Medina.

Vita vikali vilizuka nje ya msikiti wa Al-Aqsa
Vita vikali vilizuka nje ya msikiti wa Al-Aqsa
Image: REUTERS

Hatahivyo kundi la wapiganaji wa Hamas lilichukua hatua za kuionya Israel kuondoa vikosi vyake katika msikiti wa Al-Aqsa na wilaya ya Sheikh Jarrah na baadaye kurusha roketi mjini Jerusalem.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alituma ujumbe wa twitter akisema: Mashirika ya kigaidi katika eneo la Gaza yalivuka mpaka mwekundu …Israel itajibu kwa uwezo mkubwa.

Msururu mwingine wa matokeo kama hayo ungeisha vivyo hivyo. Matukio ya ghasia yatatokea mara kwa mara iwapo mzozo huo hautatatuliwa.

Je mzozo huo una suluhu?

Mtangazaji wa BBC aliniuliza hivi majuzi , wakati ambapo mzozo huo ulikuwa ukiendelea , ni lini nitakuwa na matumaini kwamba pande hizo mbili zitaafikiana mwafaka ili kuishi kwa amani.

Niliishi Jerusalem kutoka 1995 hadi 200 na nimerudi katika eneo hilo kila mara. Kupata jibu imekuwa vigumu.

Israel ilirusha mabomu kadhaa katika ukanda wa Gaza
Israel ilirusha mabomu kadhaa katika ukanda wa Gaza
Image: AFP

Katikati ya mkutano wa amani wa Oslo miaka ya 90, kulikuwa na matumaini kwa muda mfupi , lakini ni wakaazi wa Jerusalem walio katika umri wa miaka 40 ndio walio na ufahamu jinsi amani ilivyoafikiwa.

Viongozi wa pande zote mbili wamekuwa wakikabiliana kisiasa ndani ya maeneo yao , wakijaribu kulinda maslahi yao , huku tatizo kuu la kiongozi wa Palestina na Israel likiwa ni kuleta amani katika eneo hilo.

Changamoto hiyo haijaangaziwa kwa undani kwa miaka kadhaa sasa.

Mawazo mapya yamejitokeza.

Makundi mawili yanayoheshimiwa sana katika eneo la mashariki ya kati kwa kupigania amani , the Carnegie Endowment for International Peace na lile la US / Middle East Project yamechapisha ripoti ya pamoja yakisema kwamba kipaumbele ni kutoa haki sawa na usalama kwa raia wa Palestina na wale wa Israel.

Yanasema kwamba Marekani ni sharti kuunga mkono usawa kamili na haki ya kupiga kura kwa wale wote wanaoishi chini ya utawala wa Israel sio kuunga mkono mifumo tofauti isiyo na usawa wowote.