STELLA WANGU

Wakenya waadhimisha siku ya kurudi kwake Stella

Wakenya mitandaoni walichukua siku hii kushauriana na kuelimishana kutokana na masaibu yaliyompata Mwamburi

Freshley Mwamburi aliyeimba wimbo Stella
Freshley Mwamburi aliyeimba wimbo Stella
Image: HISANI: BBC

Tarehe kumi na saba mwezi wa tano huwa muhimu sana kwa Wakenya kwani kwa kawaida kuwa wameitambua kama siku halisi ya ‘Stella’ kurudi Kenya kutoka nchi ya  Japani alikokuwa ameenda kusoma.

Imekuwa kawaida Wakenya kuadhimisha ile siku ile kila mwaka kana kwamba ni sikukuu. Kilichojitokeza sana mwaka huu, Wakenya walionekana kushauriana kuhusiana na hadithi ya Stella.

Kwa wimbo Stella aliouimba Freshly Mwamburi mwakani  1992 anaeleza mshangao ambao ulimpata baada ya kukuona aliyekuwa mpenzi wake akishuka ndege huku amebeba mtoto na akiwa ameandamana na mpenzi wake Mjapani.

17th may the day stellah came back #zilizopendwa #fresheleymwamburi

Nilivyompenda Stella jamani, kajitolea kwa roho moja,

nikauza shamba langu, sababu yake yeye,

Nikauza gari langu, sababu yake yeye,

Nikauza Ng'ombe na mbuzi, sababu yake yeye,

Ili apate nauli yake na pesa nyingine za matumizi, kule Japani eeh”  Mwamburi alieleza aliyomfanyia Stella ambaye alimteka baada ya kuenda Ng’ambo.

Hata baada ya machungu aliyomsababishia Stella, kwa wimbo huo Mwamburi bado anamuomba mpenzi wake kumrudia kwani bado yuampenda.

Siku ya Jumatatu Wakenya walijitosa mtandaoni kutoa hisia zao kuhusu wimbo Stella huku kwa upande mmoja wengine wakishauri wanaume dhidi ya kujitoa muhanga ili kufurahisha wanawake na upande mwingine wengine wakiwasuta wanaume wanafanya makuu ili wanawake wawapende.

Kauli ya Stella ni funzo kuu kuwa wanawake hawajali kamwe kuhusu kujitolea kwa wanaume!” @_fels1 aliandika kwenye mtandao wa Twitter.

@hylinne aliandika “Stella wangu ni wimbo wa kimapenzi na chuki zote pamoja. Funzo kuu ni usimlipie yeyote karo kwa jina la mapenzi. Wajibika kwa watoto wako, ndugu na familia yako tu. Wengine watakuvunja moyo

Hata hivyo, wengine walionekana kutetea tendo la Stella

@Anita_Wangarii aliandika “Kauli ya Mwamburi ni funzo lilitolewa vizuri. Wanaume msiwai lipia wanawake karo, bili na nauli za ndege mkingoja mapenzi

Hizi hapa baadhi ya hisia za Wakenya.

Wakenya walitoa hisia zao mbalimbali wakilinganisha hadithi ya Mwamburi na madai ya wanawake kula nauli walizotumiwa na wanaume, tukio ambalo limekuwa maarufu nchini kwa muda sasa. 

Wengine walionekana kutumia siku hiyo kutengeza chapisho za ucheshi almaarufu kama ‘Memes’  zinazohusu hadithi ya Mwamburi na Stella.