Makali ya corona:Watu 469 wapatikana na corona huku wagonjwa 108 wakiwa Icu

Muhtasari
  • Idadi ya visa vya maambukizi ya corona nchini imefika 166,006 baada ya watu wengine 469 zaidi kupatikana na virusi hivyo
  • Maambukizi hayo mapya yalitoka kwa sampuli 6,244 zilizopimwa saa 24 zilizopita

Idadi ya visa vya maambukizi ya corona nchini imefika 166,006 baada ya watu wengine 469 zaidi kupatikana na virusi hivyo.

Maambukizi hayo mapya yalitoka kwa sampuli 6,244 zilizopimwa saa 24 zilizopita.

Kesi hizo mpya zinajumuisha Wakenya 363 na raia wa wageni 106 mgonjwa wa umri wa miaka 2 na mwenye umri wa juu ana miaka 102.

Wizara ya afya  imethibitisha kuwa vifo 8 zaidi vilirekodiwa huku idadi ya walioaga dunia kutokana na corona ikifika 3,021.

Pia watu 43 wamepona corona huku idadi jumla ya walipona ikifika 113,917.

Vifo 3 vilirekodiwa katika tarehe tofauti huku 5 vikirekodiwa kutoka kwa ukaguzi wa vituo vya afya huku 8 wakiaga dunia katika saa 24 zilizopita.

Wagonjwa 1,039 kwa sasa wamelazwa katika vituo anuwai vya afya wakati 4,714 wamo katika mpango wa huduma ya nyumbani.

Wagonjwa 108 wamo katika ICU, 22 kati yao walikuwa kwenye msaada wa upumuaji, 71 kwenye oksijeni ya ziada na wengine 15 wakichunguzwa Wagonjwa wengine 91 walikuwa kando na oksijeni ya ziada kati yao 87 walikuwa katika wadi za jumla na 4 katika kitengo cha utegemezi.