SIASA ZA 2022

Wajane wamezea mate viti vilivyoachwa na mabwana wao

Uchaguzi mdogo wa Juja na Bonchari kutumika kama kupimo cha ushawishi wa Ruto, Raila na Uhuru katika maeneo ya Kiambu na Kisii

Muhtasari

•Mjane wa Francis Waititu na Oroo Oyiaka ni kati ya wagombea viti vya ubunge

•Uchaguzi mdogo kufanyika Jumanne

Susan Njeri, mjane wa aliyekuwa mbunge wa Juja Francis Munyua.
Susan Njeri, mjane wa aliyekuwa mbunge wa Juja Francis Munyua.
Image: JOHN KAMAU

Kura za kuamua nani watakaojaza nafasi mbili zilizoachwa mbungeni baada ya aliyekuwa mbunge wa Juja marehemu Francis 'Wakapee' Waititu na Oroo Oyioka wa Bonchari kuaga zinatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne.

Maeneo bunge hayo mawili yamealika wagombea viti wasipongukia kumi kila eneo.Siku ya Jumatatu, tume la uchaguzi na mipika(IEBC) lilisambaza vifaa vitakavyotumika kwenye uchaguzi katika maeneo bunge hayo mawili.

Kinachoonekana kujitokeza katika maeneo hayo mawili ni namna wajane wa wabunge hao wawili kuwa miongoni mwa wagombeaji.Katika eneo bunge la Juja, Susan Njeri Waititu ataipeperusha tikiti ya Jubilee ilhali upande wa Bonchari Teresa Bitutu Oyioka ataipeperusha bendera ya UDA inayohusishwa na naibu rais William Ruto.

Uchaguzi huo wa Juja na Bonchari pia unatazamiwa kutumika kama kipima boriti cha kubainisha umaarufu wa Rais Uhuru Kenyatta na naibu rais William Ruto katika maeneo ya Kiambu na Kisii.

Jubilee na UDA zinawaunga wagombeaji tofauti kila mmoja.Uhasama baina ya vyama hivyo viwili umeonekana hapo awali kwenye uchaguzi ndogo zilizofanyika Msambweni, Kabuchai, Matungu na London Ward.

Naibu rais William Ruto amekuwa akitumia chama chake cha UDA kutia umaarufu wake kabiro kabla ya uchaguzi mkuu mwaka ujao. Vyama vya Jubilee na UDA vimekuwa vikipimana nguvu kwa muda sasa huku wabunge wanajihusisha na UDA wakiomba kujitenga na chama tawala cha Jubilee.

Katika eneo bunge la Juja, Susan Njeri wa Jubilee na George Koimburi wa PEP inayoungwa mkono na chama cha UDA wanadaiwa kuwa na ushawishi mkubwa ikilinganishwa na wagombea kiti wengine.

Katika eneo la Bonchari, vyama vya Jubilee, UDA na ODM vinamenyana kuona chama gani ina ushawishi mkubwa eneo hilo.