MAUAJI YA BASHIR

Uchunguzi: Mwanabiashara Msomali-Mmarekani alinyongwa

Mwili wa Mohammed Bashir ulikuwa na ishara za kuteswa zikiwemo ishara kadhaa za kugongwa na chombo butu kichwani na vidonda vya kuchomwa mwilini

Muhtasari

•Mwili wa Mohammed Bashir ulikuwa na ishara za kuteswa  zikiwemo ishara kadhaa za kugongwa na chombo butu kichwani na vidonda vya kuchomwa mwilini

Chumba cha kuhifadhia maiti cha Umash
Chumba cha kuhifadhia maiti cha Umash
Image: HISANI: The Star

Uchunguzi wa mwili wa mwanabiashara msomali-mmarekani aliyepatikana ameuliwa Mwea umeonyesha  kuwa marehemu alinyongwa hadi akafa.

Uchunguzi ule uliofanywa na mtaalam mkuu wa upasuaji  wa serikali, Johansen Oduor ulionyesha kuwa Mwili wa Mohammed Bashir, 36,  ulikuwa na ishara za kuteswa ikiwemo ishara kadhaa za kugongwa na chombo butu kichwani na vidonda vya kuchomwa mwilini. Ishara za kuteswa zilionekana kwenye miguu na vidole.

Ripoti ilionyesha kuwa vidonda vile vilikuwa na umbo la mviringo ishara kuwa zilikuwa zimewekwa kwa kutumia  lighter ya gari.

Shughuli ya upasuaji ilifanyika katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Umash kilicho Nairobi. Familia, wakili wa familia na maafisa wa DCI ni baadhi ya waliohudhuria shughuli hiyo.

Wakili wa familia, Charles Madowo alisema kuwa serikali ya Marekani ilikuwa imetuma agenti wa FBI kusaidiana na DCI kufanya uchunguzi zaidi ili kubaini amna mwanabiashara huyo alitekwa nyara. Alisema kuwwa watatoa ombi kwa DPP kuanzisha uchunguzi ili kubaini kilichosababisha kifo cha Bashir.

Mwili wa Bashir ulipatikana katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Kerugoya Level 5 baada ya marehemu kutoweka tarehe 13 Mei. Mwili huo ulikuwa umetupwa kwenye mto wa Nyamindi, Mwea na kupatikana tarehe 16 Mei.