MAAMUZI YA BBI

Mahakama ya kukata rufaa yakubali ombi la kufanya dharura kesi ya BBI

Mahakama ya kukata rufaa imeidhinisha kuwa dharura ombi la kupinga maamuzi ya mahakama kuu dhidi ya mchakato wa BBI huku rais Kenyatta pia akiwasilisha ilani ya kukata rufaa maamuzi hayo

Muhtasari

•Rais Kenyatta amewasilisha ilani ya kukata rufaa akisema kuwa hajatosheka na uamuzi wa mahakama kuu kuhusiana na mchakato wa BBI na ana nia ya kukata rufaa.

•Mahakama ya kukata rufaa imeidhinisha kuwa dharura ombi la kupinga maamuzi ya mahakama kuu dhidi ya mchakato wa BBI 

court
court

Mahakama ya kukata rufaa imekubali kufanya dharura ombi llililowasilishwa kupinga maamuzi ya mahakama kuu dhidi ya mchakato wa BBI .

Mahakama hiyo imeagiza warufani wafaili na kuwasilisha barua za mawasilisho ya kupinga uamuzi huo yaliyoandikwa wakisubiri rais wa mahakama ya kukata rufaaa aliyechaguliwa siku ya Jumapili, Daniel Musinga kuteua benchi ya kuskiza kesi hiyo.

Mwanasheria mkuu wa serikali,jopo la mchakto wa BBI na warufani wengine wameagizwa kuwapa wahojiwa mawasilisho yao mara moja.

Warufani wajaze na kuwapa wahojiwa barua za mawasilisho ndani ya siku tatu toka leo(Jumanne) ili wahojiwa nao wajibu kwa  kuwasilisha mawasilisho yao yaliyoandikwa siku tatu baadae” Mahakama iliaandikia wahusika katika kesi hiyo kupitia barua pepe.

Mahakama pia imewaagiza wahusika wote katika kesi ile kuwasilisha mawasilisho yasiyozidi kurasa tatu.

Kwa wakati huo huo, Rais Kenyatta aliwasilisha ilani ya kukata rufaa huku akisema kuwa hajatosheka na uamuzi wa mahakama kuu kuhusiana na mchakato wa BBI na ana nia ya kukata rufaa.

Kupitia wakili wake, Waweru Gatonye, rais alisema kuwa  wanapinga maamuzi hayo kwani majaji waliskiza na kuamua kesi dhidi ya BBI bila kuhakikisha kuwa alikuwa amepewa mawasilisho mwenyewe.

Gatonye alisema kuwa wanapinga uamuzi uliosema kuwa rais mwenyewe hakuhudhuria kesi na hakujaza pingamizi yoyote kuhusu uendelezaji wa kesi hiyo.