UONGOZI WA GEMA

Wazee wa Agikuyu kufanya ibada ya kutakasa hekalu

Makundi ya wazee yalisema kuwa hafla ya kutawaza Muturi ilikuwa chukizo na ilifanywa na kikundi cha wazee waasi

Muhtasari

•Makundi ya wazee yalisema kuwa hafla ya kutawaza Muturi ilikuwa chukizo na ilifanywa na kikundi cha wazee waasi

• Makundi hayo ya wazee vilisema kuwa kiongozi na msemaji wa eneo hilo alibaki kuwa Rais Kenyatta

Wazee wa Agikuyu wakitoa ujumbe wao katika makao makuu ya Kikuyu Council of Elders, Ruaka
Wazee wa Agikuyu wakitoa ujumbe wao katika makao makuu ya Kikuyu Council of Elders, Ruaka
Image: STANLEY NJENGA

Makundi kadhaa ya wazee kutoka jamii ya Agikuyu kimekashifu kutawazwa kwa spika Justin Muturi kuwa msemaji wa eneo mlima Kenya na kuapa kufanya ibada ya kutakasa hekalu ya Mukurwe wa Nyagathanga.

Miongoni mwa makundi hayo ni pamoja na Athamaki(kikisimamiwa na Njathi wa Mbatia, Boro wa Ngara, Kariuki wa Kabui na Thiong'o wa Gitau), Kikuyu Council of Elders(Kikisimamiwa na Wachira Kago), Kiama kia Ma (Kikiongozwa na Ndungu wa Gaithuma), Atonyi (Kikiwakilishwa na Kigochi wa Waimiri , Warorua wa Kimani na Wachira Kariuki).

Kupitia ujumbe mmoja uliosomwa katika makao makuu ya baraza la wazee Wakikuyu yaliyoko Ruaka, wazee walee walisema kwa sauti moja kuwa hafla ile iliyofanyika Muranga siku ya Jumamosi haikustahili na wakaonya kuwa kutawazwa hakufai kufanyika katika hekalu ya Mukurwe wa Nyagathanga.

"Kama wazee tunaotambulika tunasema kwa sauti moja kuwa kutawazwa hakufai kufanyika katika hekalu kama ilivyofanyika ovyo na kikundi cha wazee waasi" walisema wazee wale.

Wazee wale walitangaza kuwa watafanya ibada ya kutakasa hekalu hiyo kwani iliingiwa kwa hatia na hiyo ni chukizo kwa mila ya Agikuyu.Lengo kuu ya hekalu ni maombi, hafla za kimila za Agikuyu na shughuli za kimila.

Mzee Ndung'u wa Kiama kia Ma alimsuta binamu wa Rais Kenyatta, Kung'u Muigai aliyehudhuria hafla hiyo ya kutawazwa ikisemekana kuwa alikuwa amekomeshwa kuwa mmoja wa wazee wa jamii ile.

Kiago kutoka chama cha Kikuyu Council of Elders alisema kuwa wamemualika Muturi kuketi na baraza la wazee wanaotambulika na waliopewa majukumu kuwa viongozi wa jamii.

"Tunamtambua Muturi kuwa spika wa bunge, mzee wa jamii ya Mbeere na aliyependekezwa kuwa msemaji wa eneo la Mashariki mwa mlima Kenya." Kiago alisema.

Alisema kuwa itifaki haikufuatwa na hakuna mashauriano yaliyofanyika jambo ambalo lilisababisha bumbuazika baina ya washiuka dau katika eneo hilo.

Hata hivyo, vikundi hivyo vya wazee vilisema kuwa kiongozi na msemaji wa eneo hilo alibaki kuwa Rais Kenyatta.

 

Utafsiri na Samuel Maina