'Hawakujali maslahi ya watu walemavu,'UDA yalaani vikali vurugu za polisi Meru

Muhtasari
  • UDA yalaani vikali vurugu vya polisi Meru
  • Walidai kuwa tukio hilo lilikuwa sehemu ya mwenendo unaoendelea wa kuwasumbua wanasiasa wa UDA

Polisi Jumatatu walitawanya mkutano wa watarajiwa wa chama cha UDA kinachounganishwa na naibu rais William Ruto huko Meru.

Bosi wa polisi wa eneo hilo alisema wawaniaji hawakuwa na kibali cha kufanya mkutano wa ukumbi wa mji.

Baada ya tukio hilo, Naibu Rais William Ruto aliunga mkono chama hicho alilaani polisi akiwatuhumu kwa unyanyasaji na kutumia risasi za moto kutawanya kikundi hicho.

Chama hicho kilimtaka  Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai aachane na matumizi yasiyofaa .

Walidai kuwa tukio hilo lilikuwa sehemu ya mwenendo unaoendelea wa kuwasumbua wanasiasa wa UDA na wafuasi wao kama vile ilivyoshuhudiwa katika uchaguzi mdogo wa wadi ya Bonchari na Rurii.

"Kitendo cha leo ni sehemu ya mwenendo unaoendelea wa polisi kuwanyanyasa UDA na wafuasi wake kama ilivyoshuhudiwa hivi karibuni wakati wa uchaguzi mdogo katika eneo bunge la Bonchari na wadi ya Rurii huko Nyadarua. Tunalaani vikali usumbufu haramu wa mkutano wa kawaida wa UDA. "

Kupita kwa taarifa iliyoandikwa na chama hicho, walidai kwamba polisi hao hawakujali maslahi ya watu walemavu ambao walikuwa wamehudhuria mkutano huo.

"Hawakujali maslahi ya watu walemavu, ambao walikuwa wamehudhuria mkutano huo, huu mkutano ulikuwa sawa na  ile mikutano ambayo imekuwa ikifanyika katia kaunti tofauti nchini,"