Soma ujumbe wake waziri wa Uganda kwa taifa kabla ya kushambuliwa na watu wasiojulikana

Muhtasari
  • Soma ujumbe wake waziri wa Uganda kwa taifa kabla ya kushambuliwa na watu wasiojulikana
  • Washambuliaji walitoroka kwa pikipiki zao baada ya kutekeleza shambulio hilo
Waziri Edward Katumba
Image: BBC

Watu wenye silaha wamemshambulia na kumjeruhi Waziri na Kamanda wa zamani wa jeshi la Uganda, na kumuua binti yake na dereva.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema washambuliaji ambao hawajafahamika walliokuwa kwenye pikipiki walifyatua risasi kadhaa kwenye gari alimokuwa Jenerali Katumba Wamala.

Shambulio hilo limeonekana kama jaribio la kumuua kamanda huyo wa zamani wa jeshi na Mkuu wa zamani wa polisi ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ujenzi na Uchuku na limemewashtua wengi nchini Uganda.

Kuna takriban mashimo saba ya risasi kwenye dirisha la gari la Jenerali Katumba Wamala. Binti yake na dereva wote wameuawa.

Washambuliaji walitoroka kwa pikipiki zao baada ya kutekeleza shambulio hilo.

Picha ya video kutoka kwenye eneo la tukio inamuonesha Jenerali Wamala huku nguo zake zikiwa zimejaa damu –akibebwa kwenye pikipiki na kukimbizwa hospitalini.

Kabla ya mashambulio hayo waziri huyo alikuwa amewatakia wananchi wa Uganda mwezi wenye furaha na afya njema.

Pia aliwakumbusha jinsi ya kufuata kanuni za wizara ya afya ili kudhibiti maambukizi ya corona.

"Nawatakia mwezi wa Furaha, Mafanikio, Amani, Ustawi, Afya njema, na Utajiri.kukaa kwa umbali wa mita moja, kusafisha mikono, na pia kunawa mikono mara kwa mara,' Aliandika wamala.