MAPINDUZI MALI

AU yatenga Mali baada ya mapinduzi ya kijeshi

Naibu Rais wa zamani, Assimi Goita , kanali aliyeongoza mapinduzi ya Agosti na ya wiki iliyopita alitangazwa kuwa rais siku ya Ijumaa.

Muhtasari

•Jumuia ya ECOWAS ilisitisha nchi ya Mali siku ya Jumapili.

•Jeshi la nchi hiyo lilimkamata rais Bah Ndaw na waziri mkuu Moctar Ouane na kuwashinikiza kujiuzuru 

Muungano wa Africa(AU) umesitisha uanachama wa  nchi ya Mali baada ya mapinduzi ya kijeshi  yaliyotokea wiki iliyopita.

Kupitia ujumbe uliotolewa siku ya Jumanne, muungano huo pia umetishia kutoa adhabu zaidi iwapo serikali inayoongozwa na raia wa kawaida haitarejeshwa.

Wiki iliyopita, jeshi la nchi hiyo lilimkamata rais Bah Ndaw na waziri mkuu Moctar Ouane na kuwashinikiza kujiuzuru na kuzorotesha kuwepo kwa uchaguzi wa kidemokrasia baada ya uongozi uliokuwa hapo awali kupinduliwa na wanajeshi mwezi Agosti mwaka uliopita.

Naibu Rais wa zamani, Assimi Goita , kanali aliyeongoza mapinduzi ya Agosti na ya wiki iliyopita alitangazwa kuwa rais siku ya Ijumaa.

Muungano wa AU uliagiza kurejelewa kwa haraka kwa serikali inayoongozwa na raia la sivyo muungano huo utaendelea kutoa adhabu zilizolengwa.

Majirani wa Mali wanahofia kuwa mapinduzi hayo ya mwisho yatahatarishadhamira ya kufanyika kwa uchaguzi wa rais mwezi wa February mwaka ujao na kudhalilisha vita dhidi ya wanamgambo wa kiislamu katika kikanda hicho., wengine ambao wako Mali.

Jumuia ya ECOWAS ilisitisha nchi ya Mali siku ya Jumapili.

 

Tafsiri na Samuel Maina