NI MARUFUKU!

Magoha apiga marufuku mikutano inayofanyika shuleni bila idhini

Amesema kuwa mikutano hiyo inaweka wanafunzi kwenye hatari ya kuambukizwa maradhi ya Korona kwani wengi wanaohudhuria mikutano hiyo hawazingatii mikakati iliyowekwa na wizara ili kuzuia maambukizi.

Muhtasari

•"Wizara alitangaza kuwa ni marufuku kufanyia mikutano isiyoidhinishwa kwenye nyanja ama vyumba vya shule yoyote. Tuwaruhusu wasomi kuendelea na shughuli zao za kawaida bila kuwaweka kwenye hatari ya kuambukizwa maradhi ya Korona" Magoha alisema.

CS magoha
CS magoha

Waziri wa elimu nchini Prof George Magoha ametoa onyo kali kwa wanaofanyia mikutano isiyoidhinishwa ndani ya mashule.

Kupitia ujumbe kwa wanahabari uliotolewa siku ya Jumamosi, waziri Magoha amesema kuwa mikutano hiyo inaweka wanafunzi kwenye hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa Korona kwani wengi wanaohudhuria mikutano hiyo hawazingatii mikakati iliyowekwa na wizara ili kuzuia maambukizi.

"Wizara alitangaza kuwa ni marufuku kufanyia mikutano isiyoidhinishwa kwenye nyanja ama vyumba vya shule yoyote. Tuwaruhusu wasomi kuendelea na shughuli zao za kawaida bila kuwaweka kwenye hatari ya kuambukizwa maradhi ya Korona" Magoha alisema.

Magoha ameonya kuwa adhabu kali itachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka marufuku hayo.

Ameeleza kuwa wizara imesikitika kugundua kuwa kuna makundi ya watu ambayo yamekuwa yakilenga shule kama mahala pa kufanyia mikutano isiyoidhinishwa.