RIPOTI YA COVID 19

COVID 19: Visa vipya 383, wagonjwa 101 wako ICU

Watu 6,622 pekee ndio walmeweza kupata chanjo ya pili miongoni mwa 975,265 waliopokea chanjo ya kwanza

Muhtasari

•Ripoti za kuchelewa kutokana na ukaguzi kutoka vituo mbalimbali vya afya umeonyesha vifo 24 vilivyotokea kati ya mwezi wa Aprili na Mei.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe
Image: Maktaba

Watu 383 ndio wamepatika na virusi vya Corona miongoni mwa watu 3930 waliopimwa ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita na kupelekea asilimia ya maambukizi kuwa 9.7%.

Kaunti ya Kisumu inaendelea kuongoza kwa idadi ya wagonjwa wa maradhi hayo huku waathiriwa 54 wakitokea kaunti huyo. Kaunti ya Nairobi imefuata kwa karibu ikiripoti visa 53.

Wagonjwa 33 wameweza kupona. 18 baina yao walikuwa wamelazwa katika vituo vya afya mbalimbali nchini huku 15 wakipona kutoka manyumbani mwao. Idadi hii imepelekea idadi ya waliopona kufikia sasa kuwa 117,502.

Hata hivyo, ripoti za kuchelewa kutokana na ukaguzi kutoka vituo mbalimbali vya afya umeonyesha vifo 24 vilivyotokea kati ya mwezi wa Aprili na Mei. Kwa sasa idadi ya vifo vilivyoripotiwa nchini kutokana na maradhi hayo imefikia 3264.

Kwa sasa wagonjwa 1184 wamelazwa katika vituo mbalimbali vya afya huku wagonjwa 4942 wakiendelea kutibiwa kutoka manyumbani mwao. Wagonjwa 101 wako kwenye vyumba vya wagonjwa mahututi

Watu 975,265 wameweza kupokea chanjo kufikia sasa huku 295,486 baina yao wakiwa watu waliofikisha umri wa miaka 58, watu 277,776 ni wahudumu wa afya, walimu 153,089 na maafisa wa usalama 82,720.

Watu 6,622 pekee ndio walioweza kupokea chanjo ya pili kufikia leo huku 4,046 miongoni mwao wakiwa wahudumu wa afya, 1,101 ni watu waliofikisha miaka 58, walimu 445 na maafisa wa usalama 321.