Covid-19: Watu 148 wapatikana na corona, 631 wapona,21 waaga dunia

Muhtasari
  • Kenya imerekodi visa  148 vipya vya maambukizi ya corona, kutoka kwa sampuli 2,163 zilizopimwa chini ya saa 24
Waziri wa afya Mutahi Kagwe

Kenya imerekodi visa  148 vipya vya maambukizi ya corona, kutoka kwa sampuli 2,163 zilizopimwa chini ya saa 24.

Kati ya visa hivyo 144 ni wakenya huku 4 wakiwa raia wa kigeni, pia 79 ni wanaume huku 69 wakiwa ni wagonjwa wa kike.

Mgonjwa wa umri wa chini ana mwaka mmoja huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 87.

Kufikia leoo kenya imesajili  idadi jumla  ya 172,639 visa vya maambukizi ya cocona, kutoka kwa jumla sampuli ya 1,836,410.

Kaunti ya Nairobi imerekodi visa 48, Homabay visa 46, mombasa visa 8 huku Uasin Gisgu ikirekodi visa 6.

Kulingana na twakimu za wizara ya afya watu 631 wamepona corona na kufikisha idadi jumla ya 118,226 ya watu waliopona corona.

Watu 496 wamepona huku wakipokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali  135 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Kuna wagonjwa 1,147 waliolazwa hospitalini huku wagonjwa 4,802 wakipokea matibabu wakiwa nyumbani.

Watu 21 wamepona virusi vya corona na kufikisha idadi jumla ya 3,308 watu walioaga dunia.

 Vile vile kuna wagonjwa 102 ambao wamelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi ICU.

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya kwanza imefika 975,835, huku idadi ya waliopokea chanjo ya pili ikifika 13,194.