CHANJO YA COVID 19

Marekani kupatia Bara Afrika msaada wa dozi milioni 5 za chanjo ya COVID 19

Asilimia 2% pekee ya watu katika bara la Afrika ndio wamepokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya COVID 19 huku asilimia 0.6% pekee wakipokea dozi zote mbili.

Muhtasari

•Dozi  milioni 19  za chanjo hizo  zitasambazwa kote duniani katika awamu ya kwanza kupitia mpango wa Covax huku bara Afrika likipokea takriban dozi milioni 5 ambazo zitapatianwa kwa nchi zitakazochaguliwa na Jumuiya ya  Umoja wa Afrika(AU).

•Kufikia sasa, nchi ya Kenya imewapa watu 975,399 chanjo hiyo huku watu 8181 pekee wakipokea chanjo ya pili.

Rais mteule wa Marekani Joe Biden
Rais mteule wa Marekani Joe Biden
Image: Maktaba

Bara Afrika litapokea angalau dozi milioni 5 za chanjo dhidi ya virusi vya Corona kutoka nchi ya Amerika hivi karibuni.

Rais Joe Biden ametangaza kuwa nchi ya Marekani inatazamia kupeana misaada ya takriban dozi milioni 80 kote duniani kufikia mwisho wa mwezi wa Juni.

Asilimia 75% ya misaada hiyo ya dozi itasambazwa kupitia mpango wa COVAX huku asilimia 25% ikisambazwa kwa nchi zinazozihitaji sana .

Kwa dozi ambazo zitasambazwa kwa mpango wa COVAX, Nchi ya Marekani italenga sana Marekani ya Kusini, Kusini  mwa bara Asia na Afrika kwa usaidizi wa Umoja wa Afrika” Biden alitangaza.

Dozi  milioni 19  za chanjo hizo  zitasambazwa kote duniani katika awamu ya kwanza kupitia mpango wa Covax huku bara Afrika likipokea takriban dozi milioni 5 ambazo zitapatianwa kwa nchi zitakazochaguliwa na Jumuiya ya  Umoja wa Afrika(AU).

Ugavi wa mamilioni ya dozi hizo kwa nchi zingine ni ishara ya wajibu mkubwa wa serikali ya Amerika”. Tutasonga kwa mwendo wa kasi katika kuwasilisha dozi hizo huku tukitii sheria za Marekani na nchi zitakazopokea misaada hiyo kusafirisha dozi hizo kwa njia zilizo salama.” Biden alisema.

Asilimia 2% pekee ya watu katika bara la Afrika ndio wamepokea angalau chanjo moja ya chanjo ya COVID 19 huku asilimia 0.6 pekee wakipokea chanjo zote mbili.

Kufikia sasa, nchi ya Kenya imewapa watu 975,399 chanjo hiyo huku watu 8181 pekee wakipokea chanjo ya pili.