MAHAKAMANI

Kesi ya Omtata dhidi ya uteuzi wa Sialai kama karani wa bunge itaendelea - Mahakama

Tume la PSC lilikuwa limeagiza mahakama ya ajira kutupilia kesi ambayo mwanaharakati Omtata alikuwa anapinga uteuzi wa Sialai kwa mkataba bila idhini ya bunge hata baada ya kufikisha miaka 60.

Muhtasari

•Jaji Monica Mbaru aliamuru kuwa mahakama hiyo itaendelea kuskiza kesi ya Omtata huku akisema kuwa uteuzi ni kipengele cha ajira na kwa hivyo mahakama ya ajira iko na mamlaka ya kuskiza kesi hiyo.

okiya omtata
okiya omtata
Image: Maktaba

Ombi la tume la utumishi wa umma(PSC) kutaka mahakama ya ajira kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa na mwanaharakati Okiya Omtata dhidi ya uteuzi wa karani wa bunge kuu, Michael Sialai limetupiliwa mbali.

Tume la PSC lilikuwa limeagiza mahakama ya ajira kutupilia kesi ambayo mwanaharakati Omtata alikuwa anapinga uteuzi wa Sialai kwa mkataba bila idhini ya bunge hata  baada ya kufikisha miaka 60.

Jaji Monica Mbaru aliamuru kuwa mahakama hiyo itaendelea kuskiza kesi ya Omtata huku akisema kuwa uteuzi ni kipengele cha ajira na kwa hivyo mahakama ya ajira iko na mamlaka ya kuskiza kesi hiyo.

Tume la PSC lilikuwa limesema kuwa mahakama ya ajira haikuwa na mamlaka ya kushughulikia kesi hiyo.Mahakama ilisema kuwa sheria inahitaji uteuzi wa karani wa bunge kufanyika kwa njia ya uwazi na yenye upinzani.

Mahakama ilisema kuwa Omtata alikuwa amefikia kizingiti ya kipengele cha 258 na 22 cha katiba na kwa hivyo kesi hiyo haiwezi kosolewa. Mahakama iliamuru kuwa Omtata anaweza anza mashtaka yake dhidi ya PSC.

Tume la PSC lilikuwa limesema kuwa Omtata alikuwa amepokea habari kuhusiana na uteuzi huo kwa njia haramu. Hata hivyo, mahakama ilikataa kukubali wasilisho la PSC ikidai kuwa tuhuma hizo zinaweza shughulikiwa tu kupitia usikilizwaji kamili wa koti.