NGUNJIRI AKASHIFU MARAGA NA MUTUNGA

"Maraga na Mutunga wanafaa kusalia kimya!"- Ngunjiri Wambugu

Mbunge wa Nyeri, Ngunjiri Wambugu, amedai kuwa hakimu wakuu wastaafu, Maraga na Mutunga ndio walianzisha vita kati ya idara ya mahakama na matawi mengine mawili ya serikali

Muhtasari

•“CJ Mutunga na Maraga wanafaa kunyamaza. Wao ndio sababu kuna vita kati ya idara ya mahakama na matawi mengine mawili ya serikali. Walianzisha fikra kuwa mahakama ni huru na sio kitengo cha serikali” Wambugu alisema.

•Hakimu wastaafu, Willy Mutunga na David Mapema wamekashifu Rais Kenyatta kwa kile walichosema kutumia mamlaka yake vibaya na kukosa kuheshimu idara ya mahakama.

Mbunge wa Nyeri, Ngunjiri Wambugu
Mbunge wa Nyeri, Ngunjiri Wambugu
Image: The Star

Mbunge wa Nyeri, Ngunjiri Wambugu amewaagiza Hakimu wakuu wastaafu Willy Mutunga na David Maraga kukaa kimya kuhusiana na mzozo uliopo kati ya idara ya mahakama na tawi la utendaji..

Kupitia mtandao wa Facebook, Wambugu amewalaumu wawili hao kwa vita iliyopo kati ya idara ya mahakama na matawi mengine mawili ya serikali, tawi la utendaji na bunge.

“CJ Mutunga na Maraga wanafaa kunyamaza. Wao ndio sababu kuna vita kati ya idara ya mahakama na matawi mengine mawili ya serikali. Walianzisha fikra kuwa mahakama ni huru na sio kitengo cha serikali” Wambugu alisema.

Wambugu amewasuta wawili hao akisema kuwa walijiona katika hadhi ya juu kushinda rais kwenye mpangilio  vyeo vya serikali.

Walidhani kuwa wana hadhi kubwa kushinda rais kwenye serikali. Kwa sasa wanaafikiria kuwa wanaweza tishia rais kufanya umaamuzi ambao hakubaliani nao kupitia jumbe kwa wanahabari” Wambugu alisema.

Hakimu wastaafu, Willy Mutunga na David Mapema wamekashifu Rais Kenyatta kwa kile walichosema kutumia mamlaka yake vibaya na kukosa kuheshimu idara ya mahakama.

Kwenye mahojiano na stesheni ya KTN siku ya Jumatano, Maraga alikuwa amemkashifu rais kwa kutoheshimu idara ya mahakama.

Licha ya amri za korti zilizopeanwa, rais amekuwa mgumu na anasema kuwa hatachukulia njia rahisi. Rais anafaa kufuata katiba” Maraga alisema.

Hakimu mkuu huyo mstaafu pia alikashifu upinzani huku akisema kuwa hautekelezi wajibu wake wa kupinga matendo ya rais ambayo yanakiuka katiba.

Upinzani katika nchi hii umekufa na ndio maana rais ako na ujasiri wa kufanya anachokitaka. Upinzani ambao kwa sasa uko ndani ya serikali unafaa kuwa wa kwanza kukashifu rais na kumwambia kuwa analofanya si haki” Maraga alisema.

Alisema kuwa Rais alikuwa amehukumu majaji sita ambao hakuteua bila kusikizwa huku akisema kuwa rais angefuata utaratibu uliopo wa kuondoa jaji.

“Kuna utaratibu mzuri uliopo, apisha majaji hao kisha upeleke malalamishi mbele ya kamati ya JSC. Kama aliyeteuliwa ataondolewa hata kama alikuwa wakili ama jaji mbeleni.Fuata utaratibu huo” Maraga alishauri rais Kenyatta.

Siku ya Jumanne, hakimu mkuu mstaafu Willy Mutunga aliandika ujumbe wa kumkashifu rais kwa kutumia mamlaka yake vibaya kufuatia kitendo chake cha kukosa kuidhinisha uteuzi wa majaji sita waliopendekezwa na tume ya JSC.