Koome kumkomesha Uhuru, adai uhuru wa mahakama

"Mimi ni jaji na sitaki kuingia kwenye mabishano yoyote lakini nina jukumu la kurudia msimamo huu na kumtaka (Rais) Uhuru awateue majaji sita waliosalia"

Muhtasari

"Mimi ni jaji na sitaki kuingia kwenye mabishano yoyote lakini nina jukumu la kurudia msimamo huu na kumtaka (Rais) Uhuru awateue majaji sita waliosalia"

Koome alisema Mahakama iko katika hatari ya kutekwa na idara zingine na vile vile "watu ambao sitawataja".

Jaji mkuu Martha Koome
Jaji mkuu Martha Koome
Image: MAKTABA

Jaji Mkuu Martha Koome amesisitiza wito wake kutaka majaji sita walioachwa kwenye orodha ya wale walioapishwa kuapishwa.

Akizungumza wakati wa kuapishwa kwa Daniel Musinga kama rais wa Mahakama ya Rufaa, Jaji mkuu alisema wakati huo ulikuwa mchungu, kwa sababu majaji wanne - ambao waliteuliwa kuhudumu katika mahakama ya Rufaa - hawakuwepo kwa sababu ambazo hakujua yeye .

"Mimi ni jaji na sitaki kuingia kwenye mabishano yoyote lakini nina jukumu la kurudia msimamo huu na kumtaka (Rais) Uhuru awateue majaji sita waliosalia," alisema.

Koome alisema Mahakama iko katika hatari ya kutekwa na idara zingine na vile vile "watu ambao sitawataja".

Jaji  mkuu pia alielezea wasiwasi wake kuhusu ufadhili mdogo wa Mahakama na akaelekeza usemi wake kwa Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi moja kwa moja, akisema kwamba mgao wa Shilingi bilioni 17 ulikuwa mdogo sana kati ya Bajeti ya Shilingi trilioni 3.6 iliyosomwa Alhamisi.

"Tuna mahakama zingine 26 ambazo karibu zimekamilika lakini haziwezi kukaliwa kwa sababu hakuna pesa za kuzikamilisha."

"Ikiwa inabidi tukabiliane na mrundikano wa kesi na kupitisha teknolojia ili kuongeza ufanisi na kuboresha miundombinu na kupeleka haki karibu na watu, tunahitaji fedha kutengewa idara ya Mahakama."

Koome alisema Idara ya Mahakama ilikuwa ikifanyia kazi katika "jengo la kale" ambalo lilikuwa katika hali mbaya na akashangaa kwa nini wizara ya Afya haijalitaka kuwa hatari kwa kiafya na lisilofaa kutumika.

Jaji mkuu alimpongeza Musinga na akasema alitarajia kufanya kazi naye.

Wakati huo huo, jaji wa Mahakama Kuu William Ouko alimsihi Koome atumie ustadi wa kidiplomasia kukwamua uteuzi wa majaji sita.

Rais Uhuru Kenyatta alikataa kutangaza kwa majina ya majaji sita akitoa mfano wa masuala ya uadilifu.

Aggrey Muchelule, George Odunga, Weldon Korir na Joel Ngugi walitakiwa kuhudumu katika mahakama ya Rufaa lakini majina yao hayakujumuishwa kwa orodha ya walioapishwa.  Uhuru aliandika majina ya majaji 34.

Ouko alisema, "Hali iliyopo itaathiri usimamizi wa haki. Ucheleweshaji unaosababishwa na mrundikano ni shida kubwa. Inazuia ufikiaji wa haki. Inasababisha ukosefu wa haki, inakiuka haki ya mtu binafsi ya kesi ya haki na ya haraka."

"Inawaweka wengi gerezani kwa miaka mingi bila kusikizwa kwa kesi dhidi yao."