Sita wafariki kwenye makabilano ya jaribio la wizi wa mifugo Isiolo

Muhtasari

• Washambuliaji watano kutoka upande wa Samburu na mfugaji mmoja wa Turkana waliuawa wakati wa  makabiliano ya risasi.

 
• Idara ya polisi ilitoa wito kwa jamii na eneo   hilo za wafugaji katika kuheshimu maeneo ya malisho ya kila mmoja ili kuzuia makabiliano zaidi.

Crime scene
Crime scene

Watu sita waliuawa siku ya Jumamosi katika shambulio lililofanywa na wavamizi dhidi ya wafugaji wa Turkana katika hifadhi ya wanyama ya Buffalo Springs katika Kaunti ya Isiolo.

Washambuliaji watano kutoka upande wa Samburu na mfugaji mmoja wa Turkana waliuawa wakati wa  makabiliano ya risasi.

Kulingana na Kamishna wa Kaunti ya Isiolo Herman Shambi, washambuliaji kutoka upande wa Samburu walijaribu kuiba mifugo kutoka kwa wafugaji wa Turkana ambao walijibu mashambulizi na makabiliano makali ya risasi kuanza.

Idara ya polisi ilitoa wito kwa jamii na eneo   hilo za wafugaji katika kuheshimu maeneo ya malisho ya kila mmoja ili kuzuia makabiliano zaidi.