Waziri mkuu mpya wa Israel aapa kuliunganisha taifa

Muhtasari

• Anamrithi Benjamin Netanyahu ambaye alilazimishwa kuondoka ofisini baada ya miaka 12.

• Bwana Netanyahu amehudumu kwa rekodi ya mihula mitano , mara ya kwanza kuanzia mwaka 1996 hadi 1999, na baadaye kuendelea kutoka mwaka 2009 hadi 2021.

Image: REUTERS

Waziri Mkuu mpya wa Israel Naftali Bennett ameapa kuliunganisha taifa hilo lililofadhaika na chaguzi nne katika kipindi cha miaka miwili ya kukwama kisiasa.

Alisema serikali yake "itafanya kazi kwa ajili ya watu wote", akiongeza kuwa vipaumbele vitakuwa mageuzi katika elimu, afya na kupunguza taratibu nyingi za serikali.

Mzalendo huyo wa mrengo wa kulia ataongoza muungano ambao haujawahi kutokea wa vyama vinavyoungwa mkono na wabunge katika kura ya Jumapili iliyoishia 60-59.

Anamrithi Benjamin Netanyahu ambaye alilazimishwa kuondoka ofisini baada ya miaka 12.

Bwana Bennett, kiongozi wa chama cha Yamina, atakuwa waziri mkuu hadi Septemba 2023 kama sehemu ya makubaliano ya kugawana madaraka.

Halafu atamkabidhi Yair Lapid, mkuu wa karist Yesh Atid, kwa miaka miwili zaidi.

Bwana Netanyahu - waziri mkuu wa Israeli aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi - atabaki kuwa mkuu wa chama cha mrengo wa kulia cha Likud na kuwa kiongozi wa upinzani.

Wakati wa mjadala wa Jumapili huko Knesset (bunge) huko Jerusalem, Bw Netanyahu aliahidi: "Tutarudi."

Baada ya wabunge kupiga kura katika serikali mpya ya muungano, Bw Netanyahu alimwendea Bwana Bennett na kumpa mkono.

Katika hotuba yake, Bwana Bennett, 49, alisema: "Hii sio siku ya maombolezo. Kuna mabadiliko ya serikali katika demokrasia. Ndio tu.

"Tutafanya kila tuwezalo na hakuna mtu anayepaswa kuhofu ... . "

Wawakilishi wa Wapalestina wametoa maoni kuhusu serikali mpya ya Israeli.

"Hili ni jambo la ndani la Israeli. Msimamo wetu umekuwa wazi kila wakati, tunachotaka ni serikali ya Palestina kwenye mipaka ya 1967 na Jerusalem kama mji mkuu wake," msemaji wa Rais wa Palestina Mahmoud Abbas alisema.

"Ni kazi na taasisi ya kikoloni, ambayo tunapaswa kuipinga kwa nguvu ili kurudisha haki zetu," alisema msemaji wa Hamas, kundi la Kiislam linalodhibiti Gaza.

Rais wa Marekani Joe Biden alituma pongezi zake kwa Bwana Bennett, akisema anatarajia kuimarisha uhusiano wa "karibu na wa kudumu".

Israel ilifikaje katika hatua hii ?

Bwana Netanyahu amehudumu kwa rekodi ya mihula mitano , mara ya kwanza kuanzia mwaka 1996 hadi 1999, na baadaye kuendelea kutoka mwaka 2009 hadi 2021.

Allitisha uchaguzi 2019 lakini akashindwa kupata uungwaji mkono wa kutosha ili kuunda serikali mpya ya muungano .

Kulifanyika chaguzi nyengine mbili baadaye ambazo zilikamilika bila kupata mshindi wa moja kwa moja.

Image: REUTERS

Uchaguzi wa tatu ulipelekea kuundwa kwa serikali ya muungano ambapo bwana Netanyahu alikubali kugawa mamlaka na aliyekuwa kiongozi wa upinzani Benny Gantz.

Lakini mpango huo ulishindwa kufua dafu mwezi Disemba na kusababisha uchaguzi wa nne.

Ijapokuwa chama cha Likud kilijitokeza kama chama kikubwa katika bunge la Knesset lenye viti 120, bwana Netanyahu kwa mara nyengine alishindwa kuunda serikali ya muungano na jukumu hilo likapewa bwana Lipid, ambaye chama chake cha mrengo wa kati cha Yesh Atid kilikuwa cha pili kwa ukubwa.

Upinzani uliokuwa ukipinga utawala wa Netanyahu madarakani uliongezeka , sio tu miongoni mwa vyama vya mrengo wa kushoto na ule wa kati bali pia miongoni mwa walio katika mrengo wa kulia ambavyo vina mawazo sawa na chama cha mrengo wa kulia cha Likud ikiwemo Yamina.

Serikali mpya itahudumu vipi?

Kwa muonekano serikali ya bwana Bennett itakuwa tofauti na zile za watangulizi wake katika historia ya Israel ya miaka 73.

Muungano huo unashirikisha vyama ambavyo vina tofauti kubwa ya kimawazo , na pengine kitu muhimu ni kuwepo kwa chama huru cha Kiarabu kuwa ndani ya muungano huo , Raam.

Muungano huo pia utavunja rekodi ya kuwa na mwaziri wanawake wengi zaidi .

Kushirikishwa kwa Raam na vyama vya mrengo wa kushoto ambavyo sio vya Waarabu wala Waisraeli kama kile chenye sera za Israel zinazounga mkono Palestina -Yamina na chama chengine cha mrengo wa kulia , New hope , ni vyama vinavyoungwa mkono walowezi wa Kiyahudi katika maeneo yanayokaliwa ya ukanda wa magharibi kwa mfano.

Pia huenda kukawa na ugumu kuhusu sera za kutangamana huku baadhi ya vyama vikipigania haki za wapenzi wa jinsia moja kama ndoa za wapenzi wa jinsia moja , Raam ambacho ni chama cha Kiislamu kinapinga hilo.