•Maeneo yatakayoathirika ni pamoja na jiji nzima, maeneo yanaombatana na barabara ya Mombasa, Chuo Kikuu cha Nairobi, JKIA , Industrial Area na maeneo yanayoambatana na Jogoo road.
Kampuni ya maji ya Nairobi jijini Nairobi, (Nairobi City Water & Sewerage Company )imewapatia wakazi wa maeneo tofauti ya kaunti ya Nairobi ilani ya kuwepo kwa ukame wa maji siku ya Alhamisi na Ijumaa.
Hii inatokana na utengenezaji wa barabara kuu ya kutoka JKIA kuelekea Westlands ambao unaendelea .
Kupitia ujumbe wa umma, mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo , Nahashon Muguna ametangaza kuwa watakata mferenji wa maji ulio kwenye barabara kuu ya Uhuru kuanzia thenashara asubuhi siku ya Alhamisi hadi asubuhi ya siku ya Ijumaa.
“Hii itawezesha kubadilishwa kwa mifereji mzee inayoambatana na barabara kuu ya Uhuru kati ya eneo la Museum Hill na KBC ili kuonyesha wastani wa barabara kwa mkandarasi” Muguna alisema.
Maeneo yatakayoathirika ni pamoja na jiji nzima, maeneo yanaombatana na barabara ya Mombasa, Chuo Kikuu cha Nairobi, JKIA , Industrial Area na maeneo yanayoambatana na Jogoo road.
Wakazi wa maeneo hayo wameagizwa kuhifadhi maji ili wasitatizike katika kipindi hicho.