Buriani Chris Kirubi, mfanyibiashara huyo kuzikwa kesho Jumamosi

Ibada ya wafu ya Kirubi yalifanyika siku ya Ijumaa katika kanisa la Faith Evangelistic Ministry (FEM) mtani Karen mjini Nairobi

Muhtasari

Ibada ya wafu ya Kirubi yalifanyika siku ya Ijumaa katika kanisa la Faith Evangelistic Ministry (FEM) mtani Karen mjini Nairobi

Kirubi alifariki siku ya Jumatatu, Juni 14, 2021, nyumbani kwake baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu, alikuwa na umri wa miaka 80.

Mfanyibiashara tajika nchi ni Kenya Chris Kirubi atazikwa kesho katika shamba lake eneo la Thika.

Ibada ya wafu ya Kirubi yalifanyika siku ya Ijumaa katika kanisa la Faith Evangelistic Ministry (FEM) mtani Karen mjini Nairobi.

 

Kirubi alifariki siku ya Jumatatu, Juni 14, 2021, nyumbani kwake baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu, alikuwa na umri wa miaka 80.

Kinara wa upinzani Raila Odinga aliongoza viongozi wengine kumuomboleza Kirubi. Alisema kwamba marehemu alichangia sana katika kupata mwafaka baina yake na rais mustaafu Mwai Kibaki baada ya machafuko ya kisiasa kutokana na uchaguzi wa 2007.

 

Viongozi wengine waliohudhuria maombi ya wafu ya mwenda zake Kirubi ni, Makamu wa zamani Kalonzo Musyoka na Musalia Mudavadi na kiongozi wa chama cha Ford Kenya Moses Wetangula.

Mkewe Naibu Rais William Ruto Rachel Ruto na aliyekuwa mgombea Urais Peter Kenneth pia walikuwepo.

Raila alifichua kuwa marehemu Kirubi alikuwa mmoja wa watu waliomshawishi kuingia katika makubaliano ya kisiasa na Rais mstaafu Mwai Kibaki kufuatia uchaguzi wa rais uliokuwa na utata wa mwaka 2007.

 

Kiongozi huyo wa ODM alisema ni baada ya mkutano na Kirubi ndiposa mkutano uliandaliwa kati yake na Kibaki huko Sagana na kumaliza umwagaji damu mbaya zaidi katika historia ya nchi ya Kenya.

"Miongoni mwa watu wawili ambao walinijia kufanya mazungumzo alikuwa Chris Kirubi ... yule mwingine siwezi kufichua," Raila alisema.

Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka pia alisema kwamba ni Kirubi ambaye alifanya mazungumzo naye kukubali kuwa makamu wa rais Kibaki mwaka mwaka 2008.

"Alikuja nyumbani kwangu mnamo 2008 na Peter Munga na sababu ilikuwa rahisi, lazima uchukue hatua ambayo itaokoa nchi yetu."

"Ndio jinsi nilivyokuwa makamu wa 10 wa Rais wa nchi hii," Kalonzo alisema.

Mazishi ya Chris Kirubi yataanza   itaanza saa 11 asubuhi.