MARA HEIST

Spencer, Mhasibu aliyefichua ubadhirifu katika Chuo kikuu cha Maasai Mara apigwa kalamu

Baraza la Chuo Kikuu cha Maasai Mara lilimpata na zaidi ya makosa tisa

Muhtasari

•Kati ya hatia alizopatikana nazo ni pamoja na kuwa mjeuri kwa mwajiri wake, unyanyasaji wa kimitandao, kuwakilisha mwajiri wake vibaya, kueneza maneno ya uwongo, kuchafulia mtu jina, kusema maneno ya uwongo kuhusu shule, kuchochea wafanyakaziwengine dhidi ya mwajiri wake   na kutotii amri.

•Mwezi wa Desemba mwaka wa 2019 Spenser alikuwa amejulisha stessheni ya Citizen TV kuwa alikuwa akitishiwa kazini .

Chuo kikuu cha Maasai Mara
Chuo kikuu cha Maasai Mara
Image: Maktaba

Mfanyakazi wa chuo kikuu cha Maasai Mara aliyefichua ubadhirifu uliokuwa unaendelea shuleni humo mwaka wa 2019 amefutwa kazi.

Spencer Sankale Ololchike ambaye amekuwa akihudumu kama mhasibu mkuu katika chuo hicho ameachishwa kazi baada ya mkutano wa kinidhamu kumpata na hatia ya 'utovu wa nidhamu'

Kulingana na barua ya kufutwa kazi iliyotiwa saini na mwenyekiti wa baraza la chuo kikuu cha Maasai Mara, Dkt Kennedy Ole Kerei, mkutano wa kinidhamu uliofanyika Juni 16 mwaka uliopita ulimpata na zaidi ya makosa tisa.

Kati ya hatia alizopatikana nazo ni pamoja na kuwa mjeuri kwa mwajiri wake, unyanyasaji wa kimitandao, kuwakilisha mwajiri wake vibaya, kueneza maneno ya uwongo, kuchafulia mtu jina, kusema maneno ya uwongo kuhusu shule, kuchochea wafanyakaziwengine dhidi ya mwajiri wake   na kutotii amri.

"Kufuatia hatia zilizoandikwa hapo awali, baraza limeafikia kukatiza kabisa kazi yako kwenye chuo hiki kulingana na kipengele 44(4) (d) (g) cha sheria ya uajiri" Barua hiyo ilisoma.

Sankale atalipwa mshahara wa mwezi mmoja  kufuatia ilani ya kuachishwa kazi.

Kufutwa kazi kwa spenser kunatokea karibia miaka miwili baada ya stesheni ya Citizen Tv kufichua  uhalifu uliokuwa unatendeka katika chuo cha Maasai Mara.

Makala yaliyoashiria makamu mkuu wa chuo hicho Prof Mary Walingo kuwa chanzo cha ubadhirifu uliosababisha kupotea kwa mamilioni ya pesa katika chuo hicho yalionyeshwa tarehe 1 mwezi wa Septemba, 2019.

Spenser, aliyekuwa mhasibu mkuu shuleni hiyo Wilberforce Serem  pamoja na wafanyakazi wengine wawili ambao hawakutambulishwa ndio waliaidia kufichua uhalifu uliokuwa unatendeka.

Mwaka uliopita, makamu mkuu Prof Mary Walingo alishtakiwa na kosa la kuidhinisha matumizi mabaya ya fedha za shule .

Mwezi wa Desemba mwaka wa 2019 Spenser alikuwa amejulisha stessheni ya Citizen TV kuwa alikuwa akitishiwa kazini .

Spenser ameagizwa kujaza na kurudisha karatasi ya kibali aliyopatiwa kisha kuondoka shuleni humo.