RIPOTI YA KORONA

Watu 714 wapatikana na COVID 19, vifo 10 vimeripotiwa

Jumla ya wagonjwa 285 wamepona huku 167 kati yao wakiponea hospitalini na 118 kutoka manyumbani

Muhtasari

•Kaunti za Kakamega, Kisii, Migori, Nairobi, Kisumu, Busia na Siaya ndizo zinaongoza kwa maambuzi zikiwa na wagonjwa 79, 78, 76, 74, 72, 69 na 60 mtawalia.

Kufikia leo, watu 994, 622 wamepata chanjo  huku 186,966 kati yao wakiwa wamepata chanjo zote mbili.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe

Watu 714 ndio wamepatikana na virusi vya Korona katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita kati ya watu 6,039 ambao walipimwa.

Hii inaashiria kuwa asilimia ya maambukizi kwa sasa imesimamia 11.8%.

Jumla ya watu 178,792 wamekuwa waathiriwa wa maradhi ya  COVID 19 tangu mapema mwaka uliopita.

Kaunti za Kakamega, Kisii, Migori, Nairobi, Kisumu, Busia na Siaya ndizo zinaongoza kwa maambuzi zikiwa na wagonjwa 79, 78, 76, 74, 72, 69 na 60 mtawalia.

Kaunti ya Homabay imeandikisha wagonjwa 36, Nyamira 20, Uasin Gishu 17, Bomet 14, Kericho 11, Kilifi 9, Kajiado 7, Nyeri 6, Meru 6, Elgeyo Marakwet  na Nakuru 5. Kiambu , Muranga , Nyandarua na Vihiga 4 kila moja,, Garissa, Kwale, Marsabit na Narok wawili kila kaunti huku Machakos, Makueni, Turkana, West Pokot, Baringo na Kirinyaga  zote zikiandikisha mgonjwa mmoja.

Jumla ya wagonjwa 285 wamepona huku 167 kati yao wakiponea hospitalini na 118 kutoka manyumbani. Hii inapelekea idadi ya wagonjwa waliopona tangu kuingia kwa virusi nchini kuwa 122, 631.

Habari ya kuhuzunisha ni vifo vya wagonjwa 10 vimeripotiwa kutoka hospitali mbalimbali nchini.

Wagonjwa 1073 wanaendelea kuhudumiwa kwenye vituo mbambali za afya huku wagonjwa 5,174 wakiendelea kuhudumiwa nyumbani. Wagonjwa 94 wamelazwa kwenye vyumba vya waghonjwa mahututi.

Kufikia leo, watu 994, 622 wamepata chanjo  huku 186,966 kati yao wakiwa wamepata chanjo zote mbili.

Wahudumu wa afya 51, 400, watu 50, 902 waliofikisha miaka 58 , waalimu 21, 434, maafisa wa usalama 13,600 na raia wengine 49, 630 ndio wamepata chanjo zote mbili kufikia sasa.