SIASA ZA 2022

Ruto ajipigia debe ughaibuni; UDA yazindua ofisi mpya Marekani

Kangata alitangaza kuwa chama cha UDA kitazindua ofisi zingine jinini London, Uingereza.

Muhtasari

•Ofisi hizo zilizinduliwa siku ya Ijumaa na seneta wa Murang'a Irungu Kang'ata kwenye hafla iliyohudhuriwa na baadhi ya  wafuasi walio ughaibuni huku wengine haswa walio nchini Kenya wakiitazama kupitia mitandao.

•Naibu rais allihutubia wafuasi waliokuwa wanatazama hafla hiyo kwenye  mtandao. Aliahidi kuunga mkono Wakenya walio Ughaibuni

Ofisi za UDA Marekani
Ofisi za UDA Marekani
Image: Twitter

Chama cha UDA kimeanza kujipigia debe kwa Wakenya walio ughaibuni tunapokaribia uchaguzi mkuu wa 2022.

UDA ambayo inahusishwa na naibu rais William Ruto imezindua ofisi mpya  jijini Seattle, Marekani.

Ofisi hizo zilizinduliwa siku ya Ijumaa na seneta wa Murang'a Irungu Kang'ata kwenye hafla iliyohudhuriwa na baadhi ya  wafuasi walio ughaibuni huku wengine haswa walio nchini Kenya wakiitazama kupitia mitandao.

"Jana nilizindua ofisi za UDA jijini Seattle, Marekani. shukran kwa timu iliyopanga na kwa maelfu ya wafuasi ambao walihudhuria na mamilioni ambao walitazama mitandaoni. Shukran kwa naibu rais  William Ruto kwa kupamba hafla hiyo' Kangata aliandika kwenye mtandao wa Twitter.

'UDA ni cham cha kwanza kuwa na ofisi za mawasiliano ya kitaifa jijini Seattle, Marekani. Shukran kwa Bw Kiarie Prestige kwa kazi nzuri uliyofanya" Kangata aliendelea kusema.

Naibu rais allihutubia wafuasi waliokuwa wanatazama hafla hiyo kwenye  mtandao. Aliahidi kuunga mkono Wakenya walio Ughaibuni

"Tunaamini kuwa Wakenya ambao wako ughaibuni wanafaa kuhusishwa kwenye siasa za nchi pia. Hakuna sababu inayoeleweka kuhusu mbona ughaibuni haijawakilishwa kwenye serikali"  Ruto alisema.

Ruto ambaye amekuwa akisukumwa nje ya chama cha Jubilee kuanzia mwaka wa 2018  aliahidi Wakenya walio ughaibuni kuwa ataunda wizara inayowahusisha iwapo atachaguliwa kuwa rais.

Kangata alitangaza kuwa chama cha UDA kitazindua ofisi zingine jinini London, Uingereza.