Covid-19: Watu 583 wapatikana na corona,23 waaga dunia

Muhtasari
  • Watu 583 wamepatikana na maradhi ya corona kutoka kwa sampuli 6,686 zilizopimwa ndani ya saa 24
  • Idadi jumla ya maambukizi ya corona imefika 179,876  huku jumla idadi ya sampuli ikifika 1,913,782
Waziri wa afya MUtahi Kagwe
Image: Maktaba

Watu 583 wamepatikana na maradhi ya corona kutoka kwa sampuli 6,686 zilizopimwa ndani ya saa 24.

Idadi jumla ya maambukizi ya corona humu nchini imefika 179,876  huku jumla idadi ya sampuli ikifika 1,913,782.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 561 ni wakenya ilhali 22 ni raia wa kigeni, vivle vile 316 ni wanaume ilhali 267 ni wa kike.

Pia mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 5 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 101.

Watu 85 wamepona corona na kufikisha idadi jumla ya 123,050 ya watu waliopona maradhi ya corona.

65 wamepona huku wakipokea matibabu wakiwa nyumbani, ilhali 20 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali mbali mbali nchini.

Kwa habari za kuhuzunisha watu  23 wamepoteza maisha yao kutokana na corona na kufikisha idadi jumla ya 3,484 ya watu walioaga dunia.

Kuna wagonjwa 1,098 ambao wamelazwa hospitali huku 5,669 wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani.

Wagonjwa 273 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi,