Al Shabaab: Polisi 3 wajeruhiwa baada ya kushambuliwa Mandera

Maafisa hao walivamiwa walipokuwa wanasafiri kutoka kituo cha polisi cha Wargadud kuelekea Elwak asubuhi ya Jumanne.

Muhtasari

• Dereva wa gari walimokuwa alifanikiwa kuwakwepa wanamgambo hao ila maafisa 3 waliachwa na majeraha ya risasi.

• Haya yanajiri siku moja tu baada ya wanamgambo kuua watu watatu na kuteka nyara wengine watatu katika maeneo ya Falama na Jabirar kwenye mpaka wa Kenya na Somalia.

Afisa mmoja kutoka kituo cha polisi cha Bambaholwa aonyesha jeraha alilopataa baada ya mashambulizi ya Al shabaab mnamo Juni 22, 2021
Afisa mmoja kutoka kituo cha polisi cha Bambaholwa aonyesha jeraha alilopataa baada ya mashambulizi ya Al shabaab mnamo Juni 22, 2021
Image: Hisani

Maafisa watatu wa polisi wanauguza majeraha baada ya kunusurika kifo kufuatia shambulizi la wanamgambo wa Alshabaab katika eneo la Bambahowla, kaunti ya Mandera.

Maafisa hao walishambuliwa walipokuwa wanasafiri kutoka kituo cha polisi cha Wargadud kuelekea Elwak asubuhi ya Jumanne.

Dereva wa gari walimokuwa alifanikiwa kuwakwepa wanamgambo hao ila maafisa 3 waliachwa na majeraha ya risasi.

Haya yanajiri siku moja tu baada kundi la wapiganaji wa Al Shabaab wanamgambo kuua watu watatu na kuteka nyara wengine watatu katika maeneo ya Falama na Jabirar kwenye mpaka wa Kenya na Somalia.

Wanamgambo hao walivamia lori la ujenzi na kuteka nyara dereva pamoja na wenzake kabla ya kuliteketeza.

Walishambulia lori lingine lililokuwa limebeba watu watano na kuua watatu na kuwaacha abiria wawili wa kike.

Gaidi mmoja alifariki baada ya na lori la miraa kumkanyanga wakati magaidi walijaribu kusimamisha lori hilo. Hata hivyo, lori hilo lilianguka mita chache baadae na kuwezaha magaidi hao kulifikia.

 Polisi wanaendelea kutafuta wata watatu ambao walitekwa nyara. 

Tafsiri: Samuel Maina)