Wa Muchomba ataja sababu ya kuabiri 'wheelbarrow'

Wa Muchomba amekuwa mmoja wa watetezi shupavu wa Rais Kenyatta katika eneo la Mlima Kenya

Muhtasari

Wa Muchomba alidai kuwa uamuzi wake kujiunga na mrengo wa naibu rais Wiliam Ruto  ulitokana na shinikizo za wananchi wa eneo lake la uakilishi.

Mwakilishi wa wanawake wa Kiambu Gathoni Wa Muchomba na naibu rais Wiliam Ruto.
Mwakilishi wa wanawake wa Kiambu Gathoni Wa Muchomba na naibu rais Wiliam Ruto.
Image: MAKTABA

Mwakilishi wa wanawake wa Kiambu Gathoni Wa Muchomba hatimaye ametaja sababu za kuasi dau la rais Uhuru Kenyatta na kuabiri ‘wheelbarrow’.

  Wa Muchomba alidai kuwa uamuzi wake kujiunga na mrengo wa naibu rais Wiliam Ruto (Tanga tanga) ulitokana na shinikizo za wananchi wa eneo lake la uakilishi.

Alisema mabadiliko ya kisiasa aliyoyafanya hivi majuzi yalikuwa matokeo ya "shinikizo kutoka mashinani".

"Tuko nyumbani katika taifa la Hustler. Watu wa Kiambu hawafurahii jinsi shughuli za Jubilee zinaendeshwa bila kushauriana, ”alieleza.

Wa Muchomba amekuwa mmoja wa watetezi shupavu wa Rais Kenyatta katika eneo la Mlima Kenya, na mmoja wa viongozi wa kike wenye ‘sauti kubwa’ katika mrengo wa 'Kieleweke' ndani ya chama cha Jubilee.

Picha ya Wa Muchomba akiwa katika makaazi ya Ruto iliduaza wengi huku akipongezwa na wafuasi wa tanga tanga kwa “kuona mwangaza”.