KESI YA BBI

EACC yakanusha madai kuwa walifanya oparesheni katika ofisi za wakili Khaminwa siku ya Jumamosi

Khaminwa alisema kuwa alihisi kwamba anateswa kwa sababu ya msimamo wake kuhusiana na BBI

Muhtasari

•Siku ya Jumamosi, Khaminwa alisema kuwa jamaa wawili ambao alishuku kuwa maafisa wa serikali waliingia ofisini mwake na kumhoji.

•Rais wa muungano wa mawakili nchini, Nelson Havi alisema kuwa mawakili wote ambao walikuwa wakipinga  ambao walihusika katika kupinga  BBI kwenye mahakama kuu na mahakama ya kukata rufaa huenda wakalengwa na wale ambao hawakubaliani nao.

Wakili Khaminwa
Wakili Khaminwa
Image: Maktaba

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi(EACC) imekanusha madai kuwa ilifanya operesheni katika ofisi za wakili John Khaminwa siku ya Jumamosi.

Kupitia ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa Twitter  asubuhi ya Jumapili, EACC imesema kuwa madai hayo hayana msingi.

"EACC ingetaka kuwajiulisha raia kuwa hakuna operesheni yoyote ambayo tulifanya siku ya jana. Ripoti za vyombo vya habari ambazo zinasema kuwa EACC ilitembelea ofisi za wakili John Khaminwa hazina msingi wowote" EACC ilisema.

Siku ya Jumamosi, Khaminwa alisema kuwa jamaa wawili ambao alishuku kuwa maafisa wa serikali waliingia ofisini mwake na kujaribu kumhoji.

Akizungumza na wanahabari nje ya ofisi zake, wakili huyo alisema kuwa alihisi kwamba wawili hao walikuwa wanajaribu kupata manufaa ya kifedha kutoka kwake.

"Nilihisi kuwa jamaa hao wawili walikuja hapa kunitishia na kutaka kufaidika kutokana na yale nilisema mahakamani siku ya Ijumaa kuhusiana na BBI. Ningependa kusema kuwa nasimama na yale nilisema katika mahakama ya kukata rufaa  kwani niliyoyasema ni ya kisheria, halali na ni kikweli" Khaminwa aliambia wanahabari.

Wakili Khaminwa alisema kuwa wawili hao walimuomba pesa msaidizi wake baada ya kushindwa kupata ujumbe wowote kutoka kwake. Hata hivyo, hawakupatiwa chochote.

Alisema kuwa alishuku kwamba hawakuwa na amri rasmi kutoka kwa serikali.

Rais wa muungano wa mawakili nchini, Nelson Havi alisema kuwa mawakili wote ambao walikuwa wakipinga  ambao walihusika katika kupinga  BBI kwenye mahakama kuu na mahakama ya kukata rufaa huenda wakalengwa na wale ambao hawakubaliani nao.

"Mimi kama rais wa muungano wa mawakili, nitafanya lolote kuhakikisha kuwa hakuna wakili yeyote ambaye atateswa, kuumizwa au kuuliwa kwa sababu ya kuchukua msimamo mahakamani kwa niaba ya mteja wake" Havi alisema.