Uhuru asitisha ziara ya Ukambani juu ya hofu ya Covid-19

Muhtasari
  • Rais Uhuru Kenyatta amesitisha ziara yake ya siku mbili katika eneo la Ukambani kwa kuhofia ziara hiyo inaweza kusababisha kuenea kwa Covid-19
  • Rais alikuwa atembelee mkoa huo Jumanne
Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta
Image: Maktaba

Rais Uhuru Kenyatta amesitisha ziara yake ya siku mbili katika eneo la Ukambani kwa kuhofia ziara hiyo inaweza kusababisha kuenea kwa Covid-19.

Rais alikuwa atembelee mkoa huo Jumanne.

Uhuru alikuwa ametembelea Kitui mnamo Juni 25 kwa uzinduzi rasmi wa  healu la Marian of Our Lady of Protection huko Museve.

Alikuwa amekutana na viongozi wa Ukambani katikati ya Juni.

Wiki iliyopita, kiongozi wa Wiper Democratic Movement  Kalonzo Musyoka, magavana Alfred Mutua (Machakos), Charity Ngilu (Kitui), Naibu Gavana wa Makueni Adelina Mwau na maseneta Mutula Kilonzo Jnr (Makueni) na mwenzake wa Kitui Enock Wambua walifanya mkutano wa faragha na maafisa wa ikulu

Mengi yafuata;

 

 

Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta
Image: Maktaba