Covid-19:Watu 506 wapatikana na corona,355 wapona,8 waaga dunia

Muhtasari
  • Watu 506 wamepatwa na maambukizi ya corona kutoka kwa sampuli 7,376 zilizopimwa ndani ya saa 24
  • Kutoka maambukizi hayo mapya 287 ni wanaume huku 219 wakiwa ni wagonjwa wa kike, pia 468 ni wakenya 38 ni raia wa kigeni

Watu 506 wamepatwa na maambukizi ya corona kutoka kwa sampuli 7,376 zilizopimwa ndani ya saa 24.

Kutoka maambukizi hayo mapya 287 ni wanaume huku 219 wakiwa ni wagonjwa wa kike, pia 468 ni wakenya 38 ni raia wa kigeni.

Asilimia ya maambukizi nchini leo ni 6.9%, jumla idadi ya maambukizi nchini imefika 186,959 kutoka kwa idadi jumla ya sampuli 1,996,442.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 103.

Watu 355 wamepona maradhi ya corona, 241 wamepona wakiwa nyumbani ilhali 114 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka kwa hospitali tofauti.

Idadi jumla ya watu waliopona kutoka kwa corona imefika 174,522

Kwa habari za kuhuzunisha watu 8 wameaga dunia kutokana na corona, idadi jumla ya watu walioaga dunia kutokana na corona imefika 3,705.

Kuna wagonjwa 1,128 ambao wamelazwa hospitali huku 5,392 wakipokea matibabu wakiwa nyumbani.

Wagonjwa 118 wako katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).