Covid-19: Watu 452 wapatikana na corona,128 wamo ICU

Muhtasari
  • Kenya imerekodi visa 452 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 4,876 katika muda wa saa 24 zilizopita
  • Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 187,977 kutoka kwa sampuli 2,006,662
  • Asilimia ya maambukizi ya corona imefika sasa 9.3%

Kenya imerekodi visa 452 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 4,876 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 187,977 kutoka kwa sampuli 2,006,662.

Asilimia ya maambukizi ya corona imefika sasa 9.3%.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 1,327 wamepona virusi vya corona,1,272 walipona wakiwa nyumbani huku 55 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 177,783 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 2 wameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,718 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,151 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 4,241 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 128 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU