DP Ruto - Vita dhidi ya ufisadi vyanilenga mimi

Sakata ya Aror na Kimwarer ni siasa, hakuna pesa zilipotea

Muhtasari

• Naibu rais alidai kuwepo kwa njama ya baadhi ya watu katika serikali kumhangaisha kisiasa .

• Kamata kamata 'Friday' ilikuwa siasa za kupiga vita naibu rais William Ruto.

• Naibu rais alifichua kuwa Kandarasi za Arror na Kimwarer hadi sasa hazijasitishwa.

Kamata kamata Friday ilikuwa siasa za kupiga vita naibu rais William Ruto.

Naibu rais William Ruto siku ya Jumanne alishtumu serikali kwa kutumia vita dhidi ya ufisadi kama kisingizio cha kuhujumu azma yake ya kisiasa mwaka 2022.

Katika mazungumzo ya kipekee kwenye Radio Jambo siku ya Jumanne, Ruto alidai kwamba watu wanaolengwa katika oparesheni za kupambana na ufisadi ni wafuasi wake. Naibu rais kwa mara nyingine tena alikanusha vikali madai kuwa serikali ilipoteza mabilioni katika sakata ya mabwawa ya Arror na Kimwarer.

Alisema kwamba madai ya kuwepo kwa ufujaji wa pesa za umma katika kandarasi za ujenzi wa mabwawa hayo mawili yamechochewa kisiasa.

"kama kweli kulikuwa na sakata katika kandarasi ya Arror na Kimwarer kufikia sasa nani amefungwa, kama sio tu siasa," Ruto alisema.

Naibu rais aliongeza kuwa...." kandarasi za Arror na Kimwarer hadi sasa hazijasitishwa."

Naibu rais alikosoa madai ya rais Uhuru Kenyatta kwamba ufisadi ulisheheni serikali ya Jubilee miaka mitano ya kwanza akishikilia kwamba serikali iliendeshwa kwa uazi mno katika kipindi cha kwanza kabala ya "handshake" kuvuruga mipango.

"Marafiki wetu wa NASA walikuja kuharibu mipango ya Jubilee kujitafutia vyeo," Ruto alisema.

Ruto alihoji kuwa kama sio kwa sababu za kisiasa..."kwanini waliohusika katika sakata ya KEMSA ambapo mamilioni ya pesa yalipotea bado hawatiwa mbaroni..." akisisitiza kwamba hakuna pesa zilizopotea katika kandarasi ya Arror na Kimwarer.

Alidai kuwepo kwa njama ya baadhi ya watu katika serikali kumhangaisha kisiasa na kumwekea madai ya ufisadi kwa lengo la kumchafulia jina ili kusambaratisha azma yake kisiasa.

"Kulikuwa na mipango ya kuhangaisha Ruto" naibu rais alisema.

"Nimefanyiwa mambo mengi ya madharua lakini licha ya hayo sijamkosea rais...huyo jamaa ameisha ni ofisi tu ako nayo", Ruto alisema akizungumzia masaibu ambayo amekumbana nayo akiwa naibu rais katika mhula wa pili wa serikali ya Jubilee.

Alielezea hatua ya rais Uhuru Kenyatta kumpokonya majukumu na kuyapokeza mtu mwingine waziri Fred Matiang'i.

Rais Uhuru Kenyatta alimpokeza majukumu ya usimamizi wa mipango ya serikali waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang'i katika hatua iliyoonekana kama kumpokonya madaraka naibu rais William Ruto.

Kabla ya hilo naibu rais alikuwa akizuru maeneo mbali mbali ya nchi akizindua na kukagua miradi mbali mbali ya serikali hatua iliyofanya rais Kenyatta kumuita...yule kijana anayetangatanga....

Akizumunzia matamashi ya rais Kenyatta kwamba hawezi kuachia serikali mtu mfisadi, Ruto alaisema hata kama ni yeye rais hawezi kuachia serikali mtu mfisadi.

"Hata kama ni mimi rais siwezi kuachia mwizi serikali" Ruto alisema.

Alimkosoa kinara wa upunzani Raila Odinga aliyedai kwamba ikiwa atakuwa madarakani kila mtu mfisadi atakamatwa.

"Unajua kwanini Covid millionares hawajapelekwa mahali, ni kwa sababu huyo jamaa watu wake ndio walioibia wakenya", naibu rais alisema akijibu matamshi ya Raila.

Ruto ambaye alieleza wazi wazi kwamba kwa sasa anafanya bidii kukiboresha chama cha UDA alisema kwamba vita dhidi ya ufisadi nchini Kenya vimeingizwa siasa akisema kwamba anasubiri ile siku vita vya ufisadi vitaendeshwa bila muingilio wa kisiasa.

"ukionekana wewe ni rafiki wa DP kesho utaona DCI kwa mlango, kuna watu wanalazimika kunitembelea usiku kwa sababu wanaogopa kutembelewa na DCI, vita vya ufisadi vinalenga DP, Ruto alidai.